Kuchapishwa kwa makala ya mandishi Muhammad Sheikh Ould Amkhtir hapo mwaka 2014 kulisababisha maandamano makubwa kote Mauritania ambayo hayakutulia ila baada ya kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,
Mahakama ya Rufaa ya mji wa Nawadibo huko kaskazini magharibi mwa
Mauritania imepasisha hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi Muhammad Sheikh
Ould Amkhtir wa nchi hiyo kwa sababu ya kuandika makala iliyomvunjia
heshima na kumtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw) hapo mwaka
2014. Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mauritania ambaye aliomba kutolewe
hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo amesema kuwa kunyongwa kwake
kutakuwa somo kwa wale wote wanaothubutu kumvunjia heshima Mtume wa
Mwenyezi Mungu.Kuchapishwa kwa makala ya mandishi Muhammad Sheikh Ould Amkhtir hapo mwaka 2014 kulisababisha maandamano makubwa kote Mauritania ambayo hayakutulia ila baada ya kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo.