IQNA

Muqawama

Waandamanaji nchini Iraq walaani jinai za Israel huko Gaza, Lebanon

21:03 - October 12, 2024
Habari ID: 3479580
IQNA - Maandamano yamefanyika katika mji mkuu wa Iraq wa Baghdad siku ya Ijumaa kulaani jinai zinazoendelea za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.

Washiriki hao walionyesha uungaji mkono kwa wananchi wa Lebanon na Palestina wakat huu wanapokabiliwa na hujuma na jinai za utawala ghasibu wa Israe. Waandamanaji hao wamesitiza kwamba jinai za utawala huo ghasibu kamwe haziwezi kuvunja muqawama (mapambano ya Kiislamu) na waungaji mkono wake.
Walitoa wito wa uingiliaji kati wa kimataifa ili kukomesha jinai za Wazayuni katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Pia wamelaani hatua ya hivi majuzi ya matusi dhidi ya kiongozi mkuu wa Kishia wa Iraq Ayatullah Ali al-Sistani.
Abu Ala al-Wilaei, Katibu Mkuu wa Vikosi vya Sayyid al-Shuhada, alihutubia mkutano huo, akisema vitisho dhidi ya Marjaa Taqlid ni kuvuka mstari mwekundu na Wazayuni wakijaribu chokochoko yoyote watapata hasara kubwa.
Kauli hiyo imekuja baada ya Kanali ya 14 ya televisheni ya mrengo wa kulia ya utawala wa Israel kuchapisha picha ya Ayatoullah Sistani kama sehemu ya orodha ya walengwa wa mauaji yanayopangwa na utawala huo jambo ambalo limevutia kuvuta hasira ya watu wa Iraqi na maafisa, akiwemo Waziri Mkuu Mohammed Shia Al-Sudani akisema njama hiyo imewaudhi  Waislamu duniani kote.
Al-Wilaei aliendelea kusema kuwa safu ya muqawama imeweza kumshinda adui Mzayuni licha ya silaha zake za hali ya juu.
Vile vile amesema harakati ya muqawama ya Lebanon imekuwa na nguvu zaidi baada ya kuuawa shahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayed Hassan Nasrallah.
Amebainisha kuwa, muqawama wa Kiislamu nchini Iraq pia umefanya operesheni na kumsababishia hasara kubwa adui Mzayuni.

4241840

Habari zinazohusiana
Kishikizo: iraq maandamano israel
captcha