IQNA

Waungaji mkono Palestina

Maandamano ya kuunga mkono Palestina na kulaani Israeli yaendelea duniani kote

16:50 - November 30, 2023
Habari ID: 3477967
TEHRAN (IQNA)- Katika muendelezo wa himaya na uungaji mkono wa ulimwengu kwa mapambano ya wananchi wa Gaza na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Israel, maelfu ya wananchi wa Pakistan wameandamana na kuelekea katika ubalozi mdogo wa Marekani.

Waandamanaji hao wamelaani hatua ya Marekani ya kuunga mkono jinai za utawala dhalimu wa Israel na mauaji ya umati ya maelfu ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa makadirio, upinzani wa kimataifa na kulaaniwa ulimwenguni jinai za Wazayuni huko Gaza ni mkubwa na ambao haujawahhi kushuhudiwa baada ya maandamano ya kulaaniwa jinai za Marekani katika Vita vya Vietnam. Ni zaidi ya nusu karne sasa dunia haijashuhudia maandamano makubwa na ya nchi nzima kama haya ya kulaani jinai za wavamizi wakiwemo Wazayuni na vilevile baada ya kupita takriban miezi miwili tangu kuanza jinai za Israel huko Gaza maandamano ya kimataifa dhidi yake yanaendelea, jambo ambalo linahesabiwa kuwa ni kushindwa vibaya kwa Marekani na utawala wa Kizayuni. Kwa muktadha huo, Waislamu wa Pakistani pia wamekiri katika maandamano hayo kwamba usitishaji vita katika ardhi ya Palestina unabainisha  ushindi wa mhimili wa muqawama.

Wananchi wa Pakistan sawa na wapigania uhuru na wapenda haki wengine duniani wameunga mkono kikamilifu matakwa ya wananchi wa Palestina na kulaani jinai za Wazayuni wa Gaza katika kipindi cha miezi miwili iliyopita. Kuhusiana na hili, chama cha madaktari nchini Pakistan kilitangaza utayarifu wa madaktari 2800 wa nchi hiyo kutumwa Gaza  kwa minajili ya kuwasaidia Wapalestina. Kwa hakika, mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali ya Pakistani yanajaribu kusaidia Gaza kwa kutuma madaktari kwa watu wa Palestina.

Hii ni katika hali ambayo, hujuma na mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel yamekwamisha kabisa shughuli za hospitali huko Gaza hususan Hospitali ya al-Shifa ambapo katika mazingira kama haya, msaada wowote ule wa kitiba kwa ajili ya wananchi wa Gaza ni muhimu sana.

Wananchi wa Pakistan wameamua kukusanya misaada yao, ama kwa njia ya watu wa kujitolea au bidhaa za msaada, kwa kutoa dawa na vifaa, na kuzituma Gaza kupitia Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Majanga ya Kimaumbile la Pakistan.

Wakati huo huo, kundi la wanafunzi kutoka mji wa Konya, Uturuki pia lilikusanyika kwa ajili ya kuwaunga mkono watoto wa Kipalestina. Talut Kerem Cengiz, Mkuu wa Baraza la Watoto la Manispaa ya Konya amesema katika hotuba yake katika hadhara hiyo kwamba, kwa karibu karne moja sasa ambapo utawala wa Kizayuni kwa kuikalia kwa mabavu Palestina umewalazimisha mamia ya maelfu ya Wapalestina kuondoka katika ardhi zao.

Aidha, kwa mtazamo wake ni kuwa, haki itapatikana lakini si kwa Wazayuni wanaoua watoto kikatili, bali kwa kuundwa dola la Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas.

Moulawi Mofleh, mtaalamu wa masuala ya kisiasa, anasema:

"Uungaji mkono wa kimataifa kwa watu wa Gaza na kulaani jinai za Wazayuni unaonyesha kwamba, mipango yote ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na kufanya mapatano na utawala huo ghasibu unaoua watoto imefeli na kugonga mwamba, na hivi sasa kwa mara nyingine tena ulimwengu, haswa watawala wanaofanya maelewano na Israel, wamefahamu kuwa, kadhia ya Palestina itatatuliwa kwa msimamo na mtazamo wa maoni ya umma kimataifa na kwamba, harakati za maridhiano hazitakuwa na msaada wowote na haziwezi kuwaokoa Wazayuni na matatizo wanayokabiliwa nayo.

Kutokana na udharura na haja ya kuongezwa na kuimarishwa umoja na mshikamano baina ya wapenda uhuru na wapigania haki hususan nchi za Kiislamu katika kuilaani Israel, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Mahathir Mohammad amesema: “Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, ili nchi za Kiislamu zimshinde Mzayuni na adui wao wa pamoja hazina njia nyingine ghairi ya kudumisha umoja, kuimarisha msingi wa ulinzi na nguvu za kijeshi.

.

3486233
captcha