IQNA

Muqawama

Shahidi Saffiedine wa Hizbullah aenziwa

22:27 - November 01, 2024
Habari ID: 3479681
IQNA –Khitma kwa ajili ya Shahidi Sayyid Hashem Safieddine, mkuu wa Halmashauri Kuu ya Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon ambaye aliuawa shahidi mapema mwezi huu, imefanyika Tehran siku ya Alhamisi.

Kikao hicho cha kusoma Qur’ani Tukufu kiliandaliwa katika Msikiti wa Imam Sadiq (AS) katika Medani ya Palestina  na kuhudhuriwa na idadi ya maafisa wakuu wa Iran, akiwemo Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf, mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Mohammad Mokhber, na Waziri wa Usalama Seyed Esmail Khatib.
Pia kulikuwa na watu wa tabaka mbalimbali waliohudhuria Khitma hiyo.
Washiriki walikuwa wamebeba bendera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na pia za harakati za muqawama za Palestina na Hizbullah huku wakitoa nara za kulaani jinai za utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Walisisitiza uungaji mkono wao usio na kikimo kwa mhimili wa muqawama
Mkuu wa Kamati ya Kuunga mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Wananchi wa Palestina Hujjatul Islam Hassan Akhtari na kaka yake Shahidi Safieddine walitoa hotuba katika hafla hiyo.
Safieddine aliuawa katika shambulizi la kigaidi la Israel  kwenye viunga vya kusini mwa Beirut mnamo Oktoba 3, 2024.

3490508

Kishikizo: hizbullah khitma
captcha