Sheikh Naim Qassem aliyasema hayo katika hotuba yake iiliyorushwa kwenye televisheni Jumamosi jioni na kubainisha kuwa, "Adui Mzayuni anataka kuangamiza aina yoyote ile ya muqawama ambayo inakabiliana na matamanio yake ya kujitanua katika eneo zima."
Ameongeza kuwa: "Ukatili wa Israel unaolenga kuangamiza harakati ya muqawamai haujafanikiwa, na hivyo kuthibitisha ukweli kwamba ukatili kama huo hauwezi kutazamwa kuwa mafanikio hata kidogo."
Amebainisha kuwa, mashambulizi kulipiza kisasi ya Hizbullah dhidi ya vitongoji haramu vya Israel katika maeneo ya kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu yalipelekea makumi ya maelfu ya wakaazi hao kutafuta hifadhi. Amesema "Uchungu pekee ambao (utawala wa Israel) umeweza kutuletea umekuwa ni kuwaua viongozi wa Muqawama."
Sheikh Qassem pia amebainisha kuwa jeshi la Israel lingeuteka mji mkuu wa Lebanon Beirut kama isingekuwa kujitolea muhanga wapiganaji wa Hizbullah.
Akiangazia kadhia ya Syria, amesema kuwa Hizbullah iliiunga mkono nchi hiyo kwa sababu mara kwa mara ilisimama kupinga njama za Israel.
Ameongeza kuwa: "Tunatumai kuwa uongozi mpya nchini Syria utaimarisha zaidi ushirikiano kati ya mataifa na serikali za Syria na Lebanon kwa msingi wa usawa na kuheshimiana."
Pia alitarajia serikali ya mpito ya Syria itautazama utawala haramu wa Israel kama adui, na kujiepusha na mpango wowote wa kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Tel Aviv
3491052