IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun

Taarifa ya Hizbullah kufuatia kuuawa shahidi Hassan Nasrallah

15:30 - September 28, 2024
Habari ID: 3479502
IQNA- Harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa ikithibitisha kuuawa shahidi katibu mkuu wake, Sayyid Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa katika shambulio la kigaidi la utawala haramu wa Israel kwenye viunga vya kusini mwa Beirut siku ya Ijumaa.

Katika taarifa Hizbullah imesema: "Mheshimiwa, bwana wa muqawama (mapambano ya Kiislamu), mja mwema, ameelekea kuwa pamoja na Mola wake ambaye ameridhika naye kama shahidi mkuu.na kiongozi shupavu, shujaa na muumini wa kweli, akiungana na msafara wa nuru wa mashahidi wa Karbala katika njia ya Mwenyezi Mungu, na akifuata nyayo za Mitume na Maimamu waliouliwa shahidi,”

"Uongozi wa Hizbullah unaahidi ... kuendeleza jihadi yake katika kukabiliana na adui [utawala haramu wa Israel], kuunga mkono Gaza na Palestina, na kuilinda Lebanon na watu wake thabiti na wenye heshima."

Kufuatia  kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, harakati ya Hizbullah imeendeleleza taarifa yake kwa salamu za rambi rambi kwa kusema: "Tunatoa mkono wa pole kwa Imamu wa Zama (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), Walii Amri wa Waislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei, mujahidina, waumini, wanamuqawama, taifa letu lenye subira na Mujahid la Lebanon, Umma mzima la Kiislamu, wapigania uhuru wote na wanaodhulumiwa duniani, na vilevile kwa familia yake...".

Hizbullah iimesema katika taarifa hiyo kwamba: Tunampongeza Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwa kupokea nishani ya juu kabisa ya Mwenyezi Mungu, nishani ya Imam Hussein, amani ya Allah iwe juu yake, kwa kutimiza matamanio yake na kupata cheo cha juu zaidi cha imani na itikadi, akiuawa kama shahidi katika njia ya Quds na Palestina. Vilevile tunatuma rambirambi na baraka zetu kwa mashahidi wenzake waliojiunga na msafara wake safi na mtakatifu kufuatia hujuma ya kihaini wa Wazayuni kwenye viunga vya kusini mwa Beirut."

Siku ya Ijumaa, ndege za kivita za Israel zilishambulia takriban majengo sita ya makazi katika kitongoji cha Haret Hreik cha Dahiyeh, kusini mwa Beirut na kuua takriban watu wanane na kujeruhi wengine 80.Taarifa ya Hizbullah kufuatia kuuawa kigaidi Sayyid Hassan Nasrallah

Mashambulizi hayo yalikuwa sehemu mashambulizi  yaliyoshahidi ya utawala katili wa Israel dhidi ya Lebanon ambayo yalianza Oktoba 7, wakati utawala huo ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza.

Tangu Jumatatu iliyopita, mashambulizi hayo ya utawala dhalimu wa Israel yamepelekea Walebanoni zaidi ya 700 kuuawa, wengi wakiwa ni wanwake na watoto.

Hizbullah imekuwa ikijibu uchokozi huo kwa operesheni nyingi za kulipiza kisasi kuzilenga ngome za kijeshi za utawala wa Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ikiwa ni pamoja na makao makuu ya shirika la kijasusi la Mossad jinni Tel Aviv.

4239154

 

 

Habari zinazohusiana
captcha