
Hizbullah ya Lebanon imeeleza katika taarifa kwamba: "Sayyid Hashem Safieddine", Mkuu wa Baraza la Utendaji la harakati hii ameuawa shahidi katika shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Beirut".
Taarifa ya Hizbullah imeendelea kusema: "tunatoa pole kwa taifa la mashahidi na mujahidina, taifa la Muqawama na ushindi, kwa kuuawa shahidi kiongozi mkubwa na shahidi mkubwa wa njia ya Quds, Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, Sheikh Sayyid Hashem Safieddine.
Taarifa hiyo ya Hizbullah imeendelea kueleza: Sayyid Hashem Safieddine alitumia muda mwingi zaidi wa maisha yake katika njia ya kuitumikia Hizbullah na Muqawama wa Kiislamu na jamii yake; na katika kipindi cha miaka mingi ya uhai wake mtukufu, kwa uwajibikaji na uwezo kamili, aliliongoza Baraza la Utendaji, taasisi na vitengo vyake.
Kwa kumalizia taarifa yake hiyo, mbali na Hizbullah kuthibitisha tena mkono wa ahadi na baia' iliotoa kwa shahidi huyo mtukufu, imesisitiza kwamba itaendeleza njia ya Muqawama na Jihadi hadi malengo yake yatakapofikiwa ya ukombozi na ushindi..