IQNA

Muqawama

Watunisia wasema tamanio la Hassan Nasrallah limetimia

10:35 - September 30, 2024
Habari ID: 3479511
IQNA - Harakati ya Watu wa Tunisia imesema kuuawa shahidi lilikuwa ni tamanio la thamani zaidi la katibu mkuu wa harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, kundi hilo la Tunisia lilisema Mwenyezi Mungu alimtimizia Hassan Nasrallah matakwa yake baada ya muda mrefu wa Jihadi na mapambano.

Ilimtaja kiongozi huyo wa Hizbullah aliyeuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Israel kuwa ni kama kito katika taji la mapambano Kiislamu au muqawama.

Shujaa wa taifa la Kiarabu na Kiislamu na watu wote mashuhuri duniani aliuawa kishahidi, ilisema taarifa hiyo.

Harakati ya Watu wa Tunisia imetoa rambirambi kwa Hizbullah, taifa la Lebanon, Umma wa Kiarabu na Kiislamu na familia ya Nasrallah kwa kumpoteza kiongozi huyo wa kipekee katika historia ya Ummah.

Iliendelea kuahidi kuendeleza njia ya milele ya shahidi katika kutetea ukweli, Palestina na Umma.

Wakati huo huo, Mohamed Ali Nafti Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amelaani vita vikali na vya mauaji ya halaiki vya utawala wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na Lebanon na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kusimamisha jinai za utawala wa Tel Aviv.

Sayed Hassan Nasrallah aliuawa shahidi katika shambulizi kubwa la anga ambalo Israel ilianzisha kusini mwa Beirut siku ya Ijumaa kwa kutumia mabomu ya kivita yaliyotolewa na Marekani.

Mashambulizi ya utawala wa Israel yanakuja katika hali ya mvutano ulioongezeka kati ya Hizbullah ya Lebanon na utawala huo ghasibu, ambayo ni pamoja na mauaji ya makamanda wakuu wa Hizbullah na kulipuliwa kwa vifaa vya mawasiliano vya harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu.

Israel imekuwa ikiilenga Lebanon tangu Oktoba 7 mwaka jana, ilipoanzisha vita vya mauaji ya halaiki kwenye Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Hizbullah imekuwa ikijibu uchokozi huo kwa operesheni nyingi za kulipiza kisasi, ikiwa ni pamoja na moja ya kombora la balestiki ya hypersonic, ikilenga ngome za jeshi la Israel.

Harakati ya Hizbullah imeapa kuendelea na operesheni zake dhidi ya Israel madhali utawala wa Israel unaendelea na vita vyake vya Gaza.

4239557

Habari zinazohusiana
captcha