IQNA

Sheikh Qassem: Haiwezekani kuipokonya Hizbullah silaha

22:40 - April 19, 2025
Habari ID: 3480562
IQNA – Katibu Mkuu wa Hizbullay ya Lebanon amepuuzilia mbali wazo la kuipokonya  harakati hiyo, silaha zake na kusema wale wanaotoa wito wa kufanya hivyo wanahudumia ajenda ya utawala wa Kizayuni wa Israel 

Akizungumza moja kwa moja kwenye televisheni siku ya Ijumaa, Sheikh Naim Qassem pia alitoa onyo kali kwa utawala wa Israel, akisema kwamba Harakati ya Muqawamai ya Lebanon (Hizbullah) ina mahaguo mengi yake katika kukabiliana na utawala huo ghasibu. 

"Tuna machaguo na hatuogopi chochote. Ikiwa mtaendelea, mtashuhudia, kwa wakati mwafaka, kile tunachoamua kufanya," alisisitiza kiongozi huyo wa Muqawama. 

"Mtu yeyote anayefikiria kuwa sisi ni dhaifu ana ndoto za mchana," ameongeza. 

Matamshi hayo yalikuja huku utawala wa Israel ukiendeleaze  ukiukaji wa kila siku wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa  mwishoni mwa mwaka jana kwa lengo la kumaliza uchokozi wa Israel dhidi ya Lebanon ambao ulisababisha vifo vya watu wapatao 4,000 katika kipindi cha zaidi ya mwaka. 

Israel ni Tishio kwa Lebanon

Sheikh Qassem pia amesema Israel ni utawala wenye lengo la kujipanua na haijaridhika na Palestina iliyo chini ya uvamizi na inataka kukalia kwa mabavu Lebanon.

Kiongozi wa Hizbullah alikumbusha kuwa Muqawama nchini Lebanon ulizaliwa kutokana na haja ya kukabiliana na uvamizi wa Israel. Ameongeza kuwa: "Muqawamai ni jibu kwa uvamizi, na ikiwa serikali ya Lebanon haiwezi kulinda ardhi na raia wake pekee, basi ni kawaida kabisa kwa Muqawama kuwepo." 

Silaha za Hezbollah zinalenga tu kukabiliana na uchokozi wa Israel, Sheikh Qassem amesema, akipinga madai kwamba silaha za upinzani zilikuwa sababu ya kuvuruga uthabiti ndani ya Lebanon. 

Kiongozi wa Hizbullah, wakati huo huo, ameonya kwamba wale wanaotoa wito wa kusitishwa silaha za Muqawama, hasa kwa nguvu, wanahudumia ajenda ya utawala wa Israeli. 

"Lengo lao ni kuunda mgawanyiko kati ya Hizbullah na jeshi," Sheikh Qassem amesema, lakini alisisitiza kwamba "hakutakuwa na mgawanyiko [kama huo]." 

"Nguvu ya Hizbullah nchini Lebanon iko katika mafanikio makubwa na yenye athari ambayo imetimiza kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita," amesema, akibainisha kuwa kujitolea kwa harakati hiyo kumezuia Israel kutekeleza malengo yake. 

3492734

Habari zinazohusiana
captcha