IQNA

Kadhia ya Palestina

Mufti wa Misri asisitiza uwajibikaji wa kidini, kimaadili kusaidia Palestina

17:40 - December 01, 2024
Habari ID: 3479831
IQNA - Mufti Mkuu wa Misri amesisitiza wajibu wa Waislamu kuhusu suala la Palestina.

"Wajibu wetu kuhusu suala la Palestina sio tu kuwahurumia (na Wapalestina) lakini ni wajibu wa kidini, kimaadili na kihistoria," Sheikh Nazir Mohamed Ayyad alisema.

Katika taarifa iliyotolewa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, amesema Waislamu wote wanapaswa kutetea haki za Wapalestina.

Suala la Palestina sio tu kuhusu watu wanaopigania uhuru wao bali linaashiria adhama na heshima ya Umma wa Kiarabu na Kiislamu.

Waislamu wanapaswa kuisaidia Palestina kwa njia zote zinazopatikana za kisiasa, kiuchumi na vyombo vya habari, amesisitiza.

Dhamiri ya binadamu leo ​​inakabiliwa na jukumu la kimaadili na kihistoria wakati watu wa Palestina wanateseka kutokana na ukandamizaji wa wavamizi, Sheikh Ayyad amesema.

Ameongeza kuwa suala la Palestina halitasahaulika.

Vile vile amemuomba Mwenyezi Mungu awasaidie watu wa Palestina na awape subira na uthabiti na kuleta ukombozi wa Msikiti wa Al-Aqsa.

Tarehe 29 Novemba ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, na ilitangazwa kwa mara ya kwanza mwaka 1977 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kama ukumbusho wa siku ambayo Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio la kugawanya Palestina mwaka 1947.

3490883

captcha