IQNA

Mapambano

Askari wa Misri aliwaua wanajeshi watatu wa utawala wa Israel

14:46 - June 05, 2023
Habari ID: 3477103
Duru za utawala wa Kizayuni wa Israel zimethibitishwa kuwa, wanajeshi watatu utawala huo wameangamizwa wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la risasi kwenye mipaka ya Misri na Palestina inayokalia kwa mabavu ambayo imepachikwa jina bandia la Israel

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa wanajeshi wake watau walipigwa risasi na kuuawa karibu na mpaka mapema Jumamosi. Taarifa zaidi zinasema afisa wa polisi wa Misri ndiye aliyewapiga risasi na kuwwangamiza wanajeshi hao wa utawala haramu wa Israel.

Jeshi la  Misri lilithibitisha kwamba mshambuliaji aliyekufa alikuwa mwanachama wa vikosi vya usalama vya Misri.

Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliyataja mauaji hayo kuwa ni shambulizi la kigaidi. "Israel iliwasilisha ujumbe wazi kwa serikali ya Misri.” alisema katika hotuba yake kwenye televisheni.

Tukio hilo la ufyatulianaji risas uliripotiwa katika kivuko cha mpaka cha Nitzana kati ya utawala haramu wa Israel na Misri. Kivuko hicho kiko takriban kilomita 40 (maili 25) kusini mashariki mwa mahali ambapo mpaka huo unakutana naUkanda wa Gaza. Eneo hilo hutumika kuagiza bidhaa kutoka Misri zinazopelekwa Israel au Ukanda wa Gaza.

Misri ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kutia saini mkataba eti wa amani na utawala bandia wa Israel baada ya makubaliano ya Camp David ya 1978. Wakati Cairo na Tel Aviv zikishirikiana kwa karibu katika masuala ya usalama, hasa kuhusu Ukanda wa Gaza, umma wa Misri unapinga kwa kiasi kikubwa uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel ambao unakalia kwa mabavu ardhi za Palestina. Wanajeshi katili wa Israel wamewaua maelfu ya Wapalestina katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni jambo ambalo limeibua hasira katika nchi nyingi za Kiarabu na Kiislamu.

3483826

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: israel palestina misri gaza
captcha