Kongamano na maonyesho yanapangwa kufanyika Januari 13-16, 2025. Wizara ya Hija na Umrah ya Saudia itakuwa mwenyeji wa mkutano huo unaokusanya mawaziri, mabalozi, wasomi, wataalamu, wanadiplomasia na wawakilishi kutoka taasisi za kibinafsi na za umma katika nchi 87.
Kikao hicho kinalenga kuimarisha ubora wa huduma zinazotolewa kwa Mahujaji Waislamu, kukuza kubadilishana uzoefu, na kukuza ushindani na uwazi miongoni mwa makampuni yanayohusika na masuala ya Hija huko Makka na Madina.
Kutakuwa na zaidi ya wazungumzaji 100, mijadala 47 ya jopo, na warsha 50 ili kushughulikia changamoto za kuimarisha huduma za Hija na kuchunguza njia za kusaidia miradi ya ubunifu katika sekta ya Hija.
Kando ya mkutano huo, maonyesho maalum ya eneo la mita za mraba 50,000 huko Jeddah yatashirikisha waonyeshaji 280 kutoka sekta mbalimbali ili kuonyesha teknolojia ya kisasa, kama vile akili ya mnemba, ili kuimarisha Hija.
3491066