IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mwanaharakati aangazia maandalizi ya mashindano ya kiaifa ya Qur'ani ya Iran

23:07 - December 21, 2024
Habari ID: 3479932
IQNA - Mtaalamu na mwanaharakati wa Qur'ani wa Iran amepongeza maandalizi ya kitaalamu ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya nchi hiyo.

Akizungumza na IQNA, Mohammad Reza Pourmoin ameashiria duru ya hivi punde zaidi la mashindano hayo yaliyofanyika katika mji wa kaskazini-magharibi wa Tabriz na kusema tukio hilo la kitaifa la Qur'ani lina vipengele vitatu bora.

Amesema leo mashindano ya Qur'ani yanayofanyika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa usimamizi   wa Shirika la Wakfu na Misaada yana vipengele vitatu muhimu vinavyowatofautisha na mashindano mengine ya Qur'ani duniani.

Kipengele cha kwanza ni kwamba ni mashindano ya kweli ambapo kuna ushindani mzuri, usawa, ushiriki wa hali ya juu, heshima kwa watazamaji, ubunifu, na uvumbuzi katika mawasiliano kwa kiwango cha juu alichosema, akiongeza kuwa yote haya yanaonyesha  kwamba mashindano ya Qur'ani nchini Iran yanafanyika kwa weledi.

Uzingatiaji wa Qur'ani nchini miongoni mwa walimu, wakufunzi, taasisi, na mashirika mbali mbali, alisema na kuongeza kuwa tahadhari hiyo ya umma inadhihirika kwa njia mbalimbali. Aidha amesema nukta ya pili ni umma wa Iran kuzingatia Qur’ani na hilo inashuhuhudiwa katika kuhudhuria mashindano.

Pourmoin alisema kipengele cha tatu bora ushirikiano wa mashirika ya kitamaduni, kijamii na utangazaji nchini kuhusu mashindano hayo.

"Ushirikiano huu sio tu kupitia Shirika la Utangazaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), ambalo lilitangaza kwa wingi habari za mashindano mwaka huu, lakini pia kutoka kwa vyombo kama vile waendeshaji wa simu, majukwaa ya mitandao ya kijamii, n.k.

Pourmoin aliendelea kusema kuwa ubora wa mashindano ya Qur'ani uko katika kiwango kizuri na cha kuridhisha.

Alieleza matumaini yake kuwa mashindano hayo yatazidi kuimarika. Duru ya mwisho ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran ilihitimishwa katika sherehe mjini Tabriz siku ya Alhamisi.

3491129

Habari zinazohusiana
captcha