IQNA

Krismasi

Rais wa Iran: Kukumbuka kuzaliwa Nabii Isa AS ni bishara njema kwa wanaodhulumiwa

17:21 - December 24, 2021
Habari ID: 3474715
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe wa pongezi kwa Kingozi wa Kanisa Katoliki Duniani na Wakristo wote duniani kwa mnasaba wa maadhimisho ya kukumbuka kuzaliwa Nabii Issa , amani ta Mwenyezi Mungi iwe juu yake –AS-na amekutaja kuzaliwa kwa Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu kuwa ni fursa ya kukumbuka ruwaza njema ya kuwapenda wanadamu na kutoa bishara njema kwa watu wanaodhulumiwa na kukandamizwa.

Sayyid Ibrahim Raisi  Ijumaa ya leo amemtumia ujumbe Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki na Wakristo wote duniani kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Nabii Issa Masih AS (Yesu) akisema kukumbuka tukio la kuzaliwa mtukufu huyo ni fursa nzuri ya kumuenzi Bibi Maryam AS na kukumbuka sifa za kimaadili na ruwaza njema ya kuwapenda wanadamu na kutoa bishara njema kwa watu wanaokandamizwa na kudhulumiwa za Issa Masih mkabala wa dhulma na ukandamizaji wa watawala madhalimu, na vilevile  matumaini ya mustakabali mwema kwa wanadamu.

Kesho Jumamosi Disemba 25, 2021, ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Nabii Issa Masih kwa mujibu wa Wakristo waliowengi.

Issa Masih AS ni mmoja wa Mitume wakubwa wa Mwenyezi Mungu ambaye ametajwa kwa heshima na taadhima kubwa sana katika Qur'ani Tukufu.

Katika Aya kadhaa, Qur'ani Tukufu inamtambulisha Issa AS  na nafasi yake kama mmoja wa Manabii wakuu waliopewa kitabu na sheria na Mwenyezi Mungu.

4023163

captcha