IQNA

Jinai za Israel

Vikosi vya Israel vilizuia adhana  katika Msikiti wa Ibrahim mara 48 mwezi Desemba

22:34 - January 03, 2025
Habari ID: 3479999
IQNA – Vikosi vya utawala vamizi wa Israel vilizuia wito wa sala kusikika katika Msikiti wa Ibrahim mara 48 mwezi Desemba, Wizara ya Misaada na Masuala ya Kidini Palestina ilifichua jana.

Vikosi vya utawala ghasibu wa Israel vilivamia Msikiti wa Al-Aqsa ulioko mjini Quds mara 22 katika kipindi hicho, iliongeza.

Katika ripoti yake ya kila mwezi, wizara ilisema kwamba vikosi vya uvamizi na walowezi waliongeza mashambulizi yao kwenye Msikiti wa Al-Aqsa, ikibainisha kwamba waziri mwenye msimamo mkali wa Israeli Itamar Ben-Gvir, alivamia msikiti huo siku ya kwanza ya sherehe ya Kiyahudi ya Hanukkah akiwa chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya utawala wa Israel. Hii ilikuwa mara ya saba kwake kuvamia eneo takatifu la Waislamu tangu alipoingia ofisini Desemba 2022.

Ilionya kwamba mashambulizi haya yanakusudia “kuimarisha uwepo wa walowezi wa Kizayuni na kuweka hali mpya, kwa kufanya ibada za Talmud kama vile kusujudu kwa pamoja, kupiga tarumbeta n.k.”

Kuhusu Msikiti wa Ibrahim katika mji wa al-Khalil (Hebron) katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, wizara ilidokumenta kwamba “vikosi vya utawala vamizi vilizuia adhana mara 48, kuvamia, kupanda juu ya paa lake na kuchukua vipimo visivyojulikana, jambo ambalo ni ukiukaji wa wazi wa utakatifu wa maeneo ya Kiislamu na uvamizi wa mali ya Waqf.”

Askari wa Israel pia walichimbua eneo hilo ili bomba la maji taka lipite juu katika ua wa msikiti, na kumshambulia mkurugenzi wa msikiti, Sheikh Moataz Abu Sneineh, kwenye vituo vya upekuzi wa kijeshi na kumzuia kupata matibabu. Vikosi vya Israel pia vilijaribu kuvuruga tukio la usomaji wa Qur’ani.

3491312

captcha