IQNA

Jinai za Israel

Israel imebomoa au kuharibu Misikiti 1000 ya Gaza mwaka 2024

20:00 - January 06, 2025
Habari ID: 3480011
IQNA-Katika mwaka uliomalizika wa 2024, wanajeshi wa utawala wa Kiziayuni wa Israel walibomoa kikamilifu Misikiti 815 na kuharibu mingine 151 katika Ukanda wa Ghaza. Hayo yameelezwa katika ripoti iliyotolewa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini ya Palestina.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maeneo 19 ya makaburi pia yalibomolewa, yakiwemo makaburi yaliyovunjiwa heshima kwa miili iliyomo ndani yake kufukuliwa.

Aidha, makanisa matatu katika mji wa Ghaza yalilengwa na kubomolewa katika mashambulizi ya jeshi la utawala ghasibu wa Israel.

Mnamo mwezi Agosti 2024 na kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Msikiti,  Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini katika Ukanda wa Ghaza iliripoti kuwa, asilimia 84 ya Misikiti ya eneo hilo la Palestina inayokaliwa kwa mabavu imebomolewa na kuharibiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

 

Kwa mujibu wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini ya Ghaza, tangu Oktoba 7, 2023 hadi ilipotolewa ripoti hiyo, mashambulizi ya vikosi vya utawala katili wa Israel dhidi ya eneo hilo lililowekewa mzingiro yamebomoa na kuharibu maelfu ya Misikiti.

Kadhalika, mashambulizi hayo ya kinyama ya utawala wa Kizayuni yamepelekea kuuawa shahidi makumi ya wanazuoni, wahubiri, maimamu, na waadhini tangu. Aidha. hujuma hizo za Israel dhidi ya Ghaza zimeripotiwa kulenga ofisi za kamati za kukusanya Zaka, madrasa za Qur'ani na makao makuu ya Benki ya Wakfu.

3491343

 

Habari zinazohusiana
captcha