IQNA

Jinai za Israel

Wajibu kwa wanadamu wote': Mufti wa Serbia ahimiza kukabili uhalifu wa Israel huko Gaza

16:42 - June 05, 2024
Habari ID: 3478934
IQNA - Mufti katika jumuiya ya Kiislamu ya Serbia anasema kukabiliana na jinai zinazoendelea za Israel huko Gaza ni jukumu la wanadamu wote.

Akizungumza na IQNA, Sheikh Senad Halitović alisema kuwa "uhalifu mkubwa" unafanyika dhidi ya watu wa Palestina, haswa huko Gaza.

"Hali hii sio tu inalemea sana mioyo ya Waislamu bali pia inaamsha dhamiri za walimwengu," aliongeza.

“Kukabiliana na uhalifu huu si jukumu la Waislamu pekee; ni wajibu kwa binadamu wote,” alisisitiza Mufti.

"Tunashuhudia kupoteza maisha ya watu wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto wa Kipalestina, na uharibifu wa miundombinu muhimu huko Gaza na utawala unaoukalia kwa mabavu na washirika wake ambao wanadai kutetea uhuru na demokrasia," alisema.

"Ni wajibu wetu kusimama katika mshikamano na watu wa Palestina, bila kujali dini tunayofuata," Halitović aliongeza.

Matamshi hayo yanajiri wakati ambapo jeshi la utawala ghasibu wa Israel limeua zaidi ya Wapalestina 36,500 tangu Oktoba 2023. Idadi kubwa ya waliouawa ni wanawake na watoto.

Kampeni hiyo ya kikatili ilizinduliwa baada ya Hamas kutekeleza operesheni yake ya kihistoria ya Kimbunga cha  Al-Aqsa ya kulipiza kisasi dhidi ya jinai za utawala haramu wa Israel.

3488624

Habari zinazohusiana
captcha