IQNA

Tuzo ya Kimataifa ya Usomaji wa Qur'ani ya Al-Ameed: Maqari wa Iran Wafuzu kwa Awamu ya Pili 

21:13 - March 16, 2025
Habari ID: 3480383
IQNA – Kufuatia hitimisho la hatua ya kwanza ya Tuzo ya 2 ya Kimataifa ya Usomaji wa Qur'ani ya Al-Ameed, waandaaji wametangaza wale waliopita hadi awamu ya pili. 

Kulingana na Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala, Iraq, washiriki 15 kati ya 30 kwenye sehemu ya watu wazima wamefuzu kwa hatua inayofuata. 

Miongoni mwao ni waqari watatu wa Iran, ambao ni Hamid Reza Moqaddasi, Rahim Sharifi na Saeed Parvizi. 

Wengine wanatoka Misri, Iraq, Indonesia, Tanzania, Morocco, Afghanistan, Uturuki, Lebanon na Ufilipino.. 

Shirika la Kisayansi la Qur'ani la idara hiyo limeandaa tukio hilo la Qur'ani huko Karbala kwa lengo la kukuza utamaduni wa Qur'ani. 

Jopo la majaji linajumuisha wataalam wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali, wakiwemo Sheikh Mohamed Basyuni kutoka Misri, Abdul Kabir Heidari kutoka Afghanistan, Muhammad Asfour kutoka Misri, Hassanayn al-Hulw kutoka Iraq, Seyed Karim Mousawi kutoka Iran na Muhammad Rammal kutoka Lebanon. 

Toleo la kwanza la Mashindano ya Kimataifa ya Usomaji wa Qur'ani ya Al-Ameed katika Ramadhani ya 2024 lilivutia washiriki kutoka nchi 21. 

3492345

captcha