IQNA

Haram ya Karbala yajiandaa kwa vikao vya Qur'ani Tukufu katika Mwezi wa Ramadhani

15:44 - February 20, 2026
Habari ID: 3481963
IQNA – Ataba (uongozi na usimamizi) wa Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS) mjini Karbala, Iraq, umetangaza kukamilika kwa maandalizi yote ya kuandaa hafla ya Khatm Qurani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Khatm Qur'ani ni ibada ya kusoma Qur'ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Katika mwezi wa Ramadhani, Waislamu kwa kawaida husoma juzuu moja ya Qur'ani kila siku, ili ifikapo mwisho wa mwezi wawe wamehitimisha kusoma Kitabu Kitukufu chote.

Hafla ya Khatm Qur'ani ya Ramadhani katika Haram ya Hadhrat Abbas (AS) hufanyika kwa msaada wa Taasisi ya Qurani Tukufu, inayohusishwa na Jumuiya ya Kielimu ya Qur'ani ya Ataba.

Mushtaq al‑Ali, rais wa Jumuiya ya Kielimu ya Qur'ani Tukufu, alisema hapo awali kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika kwa ajili ya hafla hii ya Khatm Qur'ani.

Alibainisha kuwa lengo kuu la programu hii ni kuwawezesha mahujaji na wageni watukufu kunufaika na vikao hivi vya nuru na kiroho katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa upande wake, Sheikh Jawad al‑Nasrawi, mkurugenzi wa Taasisi ya Qur'ani Tukufu, alisema kuwa wasomaji mbalimbali wa Qurani (maqari) watashiriki kwa kusoma Qur'ani kila siku katika hafla hiyo.

Jumuiya ya Kielimu ya Qur'ani Tukufu pia huandaa programu kama hizi katika misikiti na hussainiya za mji wa Karbala, pamoja na matawi yake katika miji mingine, kwa lengo la kueneza utamaduni wa Qur'ani na kuimarisha uhusiano wa jamii na Neno la Wahyi.

3496482

Habari zinazohusiana
captcha