
Mashindano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Kusimamaia Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS) mjini Karbala, Iraq, mahali penye hadhi kubwa ya kiroho katika ulimwengu wa Kiislamu.
Wasomaji wa Qur’ani kutoka mataifa ya Kiarabu, Asia na Afrika walishiriki katika tukio hilo la kimataifa, lililoandaliwa kwa nidhamu na heshima inayolingana na utukufu wa Kitabu Kitukufu.
Qari mashuhuri kimataifa, Mohsen Qassemi, alitwaa tuzo ya juu kabisa. Kabla ya ushindi huu, Qassemi alikuwa tayari ameshiriki katika mashindano mbalimbali ya Qur’ani ndani na nje ya Iran, yakiwemo mashindano ya kimataifa ya Qur’ani nchini Malaysia.
Tuzo ya Al-Ameed huandaliwa kila mwaka kabla ya kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Taasisi ya Kusimamaia Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS) katika kueneza na kuimarisha utamaduni wa usomaji wa Qurani Tukufu katika ngazi ya kimataifa.
Katika toleo la mwisho la mashindano hayo, lililofanyika mwezi Machi 2025, wasomaji wa Qurani kutoka mataifa 22 , yakiwemo Iran, Indonesia, Afghanistan, Malaysia, Afrika Kusini, India na Misri, walifanikiwa kufika hatua ya fainali.
Habari inayohusiana:
Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Haram ya Hadhrat Abbbas (AS)
Waandaaji wamesema kuwa lengo la mashindano haya ni kuimarisha mshikamano wa Qur’ani duniani, kukuza maadili ya Kitabu Kitukufu, na kuwaunganisha wasomaji kutoka pembe mbalimbali za dunia chini ya dhamira moja ya kiroho na ibada.
3496333