IQNA

Tuzo  ya Kimataifa ya Qur’ani ya Karbala: Raundi ya pili ya hatua ya awali yaanza

22:48 - May 06, 2025
Habari ID: 3480644
IQNA-Taasisi ya Dar-ol-Quran ya Idara ya Mfawidhi wa Haram tukufu ya Imam Hussein (AS) imetangaza kuanza kwa raundi ya pili katika hatua ya awali ya Tuzo ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani ya Karbala.

Wassam Nadir al-Delfi, mkuu wa ofisi ya vyombo vya habari ya Kituo cha Dar-ol-Quran, amesema raundi ya pili imeanza kwa uwepo wa jopo maalumu la majaji katika kituo cha Karbala. 

Katika hatua hii, washiriki 37 kati ya 156 walioteuliwa katika raundi ya awali wamehitimu, amebaini. 

Jumla ya watu 468 kutoka zaidi ya nchi 50 za Kiarabu na zisizo za Kiarabu walituma faili zao za sauti kwa ajili ya kitengo cha usomaji wa Qur'ani cha mashindano haya. 

Amesisitiza kuwa mashindano haya yamekuwa jukwaa la kimataifa la kugundua wenye vipaji vya Qur'ani ambao watakuwa wawakilishi bora wa Iraq na nchi za ulimwengu wa Kiislamu katika duru za kimataifa za Qur'ani. 

Aliendelea kusema kuwa mashindano haya yanahusiana na mradi wa kina wa Qur'ani wa idara hiyo ili kuimarisha utamaduni wa Qur'ani katika jamii na kusaidia vijana wenye vipaji. 

Jopo la majaji wa mashindano haya linajumuisha wataalam 6 wa Qur'ani ambao wanatathmini waombaji kwa kuzingatia kanuni za Sawt, Lahn, Maqamati ya Qur'ani, na Tajweed kwa mujibu wa vigezo vikali vya uamuzi. 

Raundi ya mwisho ya toleo la 4 la Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani ya Karbala imepangwa kufanyika ana kwa ana huko Karbala katika hafla ya Eid al-Ghadir (katikati ya Juni).

3492954

Habari zinazohusiana
Kishikizo: karbala qurani tukufu
captcha