IQNA

Raundi ya mwisho ya Tamasha la Qur’an kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Iran

15:23 - May 25, 2025
Habari ID: 3480737
IQNA – Raundi ya mwisho ya mashindano ya Qur’an kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran, toleo la 39, imeanza rasmi Jumamosi kwa hafla maalum ya uzinduzi.

Chuo Kikuu cha Mohaqqeq Aredebili kilichopo katika mji wa kaskazini-magharibi wa Ardebil ndicho  mwenyeji wa raundi hii ya fainali, ambayo itaendelea hadi Jumatatu. Takriban wanafunzi 400 kutoka vyuo mbalimbali nchini wamefuzu hadi hatua hii ya mwisho ya mashindano.

Washiriki wanachuana katika vitengo kadhaa, vikiwemo usomaji wa Qur’an (Qira’a), kuhifadhi Qur’an kwa ngazi nne tofauti, Tarteel, usomaji wa dua, pamoja na Adhana.

Jumla ya wataalamu 16 wa masuala ya Qur’an wanashiriki kama majaji, wakigawanyika kati ya vitengo vya wanaume na wanawake. 

Tamasha hili pia lina sehemu ya mashindano ya fasihi, sanaa, utafiti na ubunifu. Washindi wa nafasi tatu za juu katika kila kipengele watatangazwa na kutunukiwa zawadi maalum katika hafla ya kufunga tamasha siku ya Jumatatu.

3493214

Habari zinazohusiana
captcha