Kwa mujibu wa waandaaji, juhudi hii inalenga kuiweka tuzo hiyo miongoni mwa mashindano ya Qur’ani yanayoheshimika zaidi duniani, huku ikithibitisha nafasi ya Dubai kama kitovu cha kimataifa cha kuheshimu na kuthamini wahifadhi wa Qur’ani kutoka mataifa mbalimbali.
Toleo hili la 28 linakuja na ongezeko kubwa la zawadi, ambapo jumla ya zawadi zitazidi dirham milioni 12 (AED12M), na mshindi wa kwanza katika kila kundi (wanaume na wanawake) atapokea zawadi ya dola milioni moja za Kimarekani (USD 1M).
Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano haya, wanawake pia wamepewa fursa kupitia kundi maalum, hivyo kufanya idadi ya makundi kuwa matatu:
Kuhifadhi Qur’ani yote kwa wanaume,
Kuhifadhi Qur’ani yote kwa wanawake,
Tuzo ya Shakhsia wa Kiislamu wa Mwaka.
Toleo hili linalokuja pia litashuhudia ongezeko la ushiriki wa kimataifa, kuongezwa kwa zawadi za kifedha, maboresho katika mfumo wa uteuzi, tathmini, pamoja na fursa ya uteuzi wa kibinafsi sambamba na uteuzi rasmi wa nchi au taasisi za Kiislamu zilizoidhinishwa.
Taarifa hizi zilitangazwa rasmi katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai katika makao ya Creators HQ, Emirates Towers, Dubai.
Masharti ya ushiriki kwa wanaume na wanawake ni pamoja na:
Kuhifadhi Qur’ani yote kwa umahiri na ustadi wa Tajweed,
Umri usiozidi miaka 16 wakati wa usajili (zamani ilikuwa miaka 25),
Asiwe ameifikia hatua ya mwisho wala kutuzwa katika matoleo yaliyopita,
Kushiriki katika vipindi vya majaribio kwa mujibu wa ratiba rasmi.
Vipimo vya washiriki vitapitia hatua tatu:
Tathmini ya awali kwa njia ya video zilizopakiwa kupitia tovuti rasmi ya tuzo,
Mtihani wa mbali (remote) kwa waliopita duru ya kwanza,
Mtihani wa mwisho wa ana kwa ana, ambapo washiriki bora wataalikwa Dubai wiki ya pili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Uwasilishaji wa maombi umefunguliwa kuanzia Mei 21 hadi Julai 20.
Tathmini ya awali itafanyika Julai 1 hadi 31, 2025.
Tathmini ya pili (kwa video ya mbali) itaendeshwa Septemba 1 hadi 30.
Hatua ya mwisho (majaji na hafla ya tuzo) itafanyika wiki ya pili ya Ramadhani.
Kamati ya majaji kwa makundi ya wanaume na wanawake itajumuisha wajumbe watano: mwenyekiti, makamu mwenyekiti na mjumbe wa akiba (sita). Majaji wanapaswa kuwa wahitimu wa kuhifadhi Qur’ani, wajuzi wa kanuni za Tajweed, na waliosomea angalau qira’a saba au kumi kwa mujibu wa mahitaji.
Kundi la tatu la tuzo ni Tuzo ya Shakhsia wa Kiislamu wa Mwaka, ambayo hutolewa kwa mtu binafsi au taasisi iliyochangia kwa kiwango kikubwa katika huduma za Kiislamu na kwa Waislamu duniani. Vigezo vinajumuisha:
Athari chanya na ya kudumu katika jamii,
Mchango mkubwa wa kielimu na kihistoria,
Sifa bora za kuwa kielelezo cha kuigwa katika ulimwengu wa Kiislamu.
Mshindi wa tuzo hii pia atatunukiwa zawadi ya dola milioni moja za Kimarekani.
3493331