IQNA

Nchi 128 Kushiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Makkah

0:19 - August 09, 2025
Habari ID: 3481053
IQNA – Msikiti Mtakatifu jijini Makkah unatarajiwa kuanza kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani kuanzia Jumamosi.

Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi, Kusoma na Kufasiri Qur’ani yatapigwa kambi katika mji huo mtukufu kuanzia kesho.
Tukio hili linaandaliwa na kusimamiwa na Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Dawah na Mwongozo ya Saudi Arabia.

Washiriki kutoka nchi 128 duniani kote wanatarajiwa kushirik, dadi kubwa zaidi ya mataifa kushiriki tangu mashindano haya yaanze zaidi ya miaka 45 iliyopita.

Waziri wa Mambo ya Kiislamu, Dawah na Mwongozo, Abdullatif bin Abdulaziz Al Al-Sheikh, alisema:
“Wizara inajivunia heshima ya kuandaa mashindano haya yenye hadhi kubwa, ambayo yanachukuliwa kuwa miongoni mwa mashindano mashuhuri zaidi ya kimataifa ya Qur’ani.”

Akaongeza:
“Yanawakutanisha pamoja wahifadhi mahiri wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kutoka pembe zote za dunia, hapa katika sehemu tukufu zaidi duniani, kila mwaka.”

 

3494158

captcha