Mwaka mpya wa Kiislamu wa 1446 utaanza Jumapili, Julai 7.
Msemaji wa wizara hiyo alisema programu za mwaka ujao zitajumuisha semina na vikao zaidi ya 500 vya Qur'ani.
Idadi ya duru za Qur'ani na vikao vya kisomo pia itaongezeka kwa kiasi kikubwa, Abdullah Hassan aliongeza.
Alisema juhudi za kurejesha na kukarabati misikiti pia zitaendelea mnamo 1446.
Alibainisha kuwa takriban misikiti 12,000 kote nchini imerejeshwa na kukarabatiwa tangu 2014 kwa gharama ya karibu pauni bilioni 18 za Misri.
Katika mwaka mpya, kazi ya kurejesha itafanywa katika misikiti mikubwa 16, kulingana na msemaji huyo.
Hassan aidha amesema Khatm Quran (zinazosoma Kitabu kitukufu tangu mwanzo hadi mwisho) zimepangwa kufanyika katika misikiti ya nchi katika siku ya kwanza ya mwaka mpya kwa kushirikisha makari wakuu.
Redio ya Qur'ani ya Misri Inamkumbuka Qari Sheikh Shuaisha
Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.
Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.
Shughuli za Qur'ani ni za kawaida sana katika nchi hiyo ya Kiarabu yenye Waislamu wengi na wengi wa makari wakuu wa ulimwengu wa Kiislamu hapo awali na wa sasa wamekuwa Wamisri.