Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alikuwa mzungumzaji mkuu katika sherehe za kuzinduliwa kikao hicho.
Kongamano hili hufanyika kila mwaka wakati waWiki ya Umoja wa Kiislamu kwa mnasaba wa Maulidi au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Mtume Mtukufu Muhmmad (SAW) na huandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu. Mwaka huu, Palestina ndio mada kuu ya hafla ya mwaka huu.
Kongamano la Umoja wa Kiislamu la mwaka huu limeafanyika chini ya kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kiislamu kwa ajili ya kufikia Maadili ya Pamoja kwa kutilia mkazo Suala la Palestina." Wanazuoni wa Shia na Sunni kutoka Iran na nchi mbalimbali duniani wanashiriki katika mkutano huo.
Kulingana na waandaaji, wageni kutoka nchi 30, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Jordan, na UAE, pamoja na Marekani, Urusi, Indonesia, na wengine, wamehudhuria mkutano huo.
Programu zilizopangwa kwa wageni wa kongamano la 38 ni pamoja na kukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kutembelea vituo vya sayansi na teknolojia, kutembelea kaburi la Imam Khomeini kusini mwa Tehran, ziara ya Mnara wa Milad mjini Tehran, na kushiriki Sala ya Ijumaa.
3489967