IQNA

Mkutano wa 34 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu kujadili ushirikiano wakati wa maafa

17:19 - October 04, 2020
Habari ID: 3473231
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema Mkutano wa 34 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu utafanyika kwa njia ya intaneti na kujadili ushirikiano wakati wa maafa kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 3 kwa mnasaba wa Maulid ya Mtume Muhammad SAW na Wiki ya Umoja wa Kiislamu.

Hujjatul Islam Hamid Shahriyari Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran pembizoni mwa kikao cha kupanga na kuratibu sherehe za Maulid ya Mtume SAW na wiki ya Umoja wa Kiislamu.

"Wiki hii Wiki ya Umoja wa Kiislamu inasadifiana na Oktoba 29 hadi Novemba 3 na tuna mpango wa kuwaleta pamoja wasomi 200 kutoka kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu kuzungumza kuhusu umoja wan Umma wa Kiislamu. Mkutano huu utafanyika kwa njia ya intaneti na pia ana kwa ana katika maeneo nane ya kijiografia duniani."

Shahriari amesema sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa Umoja wa Kiislamu zitafanyika 29 Oktoba sawa na 12 Rabi ul Awwal na kumalizika 3 Novemba sawa na 17 Rabi ul Awwal.

Shahriari amesema sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa Umoja wa Kiislamu zitafanyika 29 Oktoba sawa na 12 Rabi ul Awwal na kumalizika 3 Novemba sawa na 17 Rabi ul Awwal.

Hujjatul Islam Shahriyari amesema kwa kuzingatia kuwa ulimwengu unakabiliwa na janga la corona, mwaka huu mada ya mkutano wa umoja wa Kiislamu itakuwa ni kuhusu ushirikiano wa Kiislamu wakati wa majanga na maafa.

Amesema ushirikiano wa nchi za Kiislamu katika kukabiliana na corona ulikuwa tafauti na nchi za Magharibi. "Waislamu duniani, hasa watu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wameonyesha wanaweza kukabiliana na janga hili kwa ustaarabu huku katika nchi za Magharibi kukishihudiwa matatizo mengi hasa utamaduni wa kiliberali wa ubinafsi," amesema Hujjatul Islam Shahriyari.

Mkutano huo hufanyika kila mwaka kwa munasaba wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Inafaa kuashiria hapa kuwa Wiki ya Umoja wa Kiislamu ni kipindi cha kati ya tarehe 12 na 17 za Mfunguo Sita Rabiu Awwal kipindi ambacho kinasadifiana na kuadhimisha Maulidi na kumbukumbu ya kuzaliwa Bwana Mtume SAW. Kuhusiana na kuzaliwa Bwana Mtume SAW kuna riwaya mbili mashuhuri. Waislamu wengi wa madhehebu ya Kisuni wanaamini kwamba, Bwana Mtume SAW alizaliwa tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal mwaka wa tembo uliosadifiana na mwaka 570 Miladia.

Kundi jengine la Waislamu ambalo linaundwa zaidi na Waislamu wa madhehebu ya Shiia Ithanaashari linaamini kwamba, Mtume wa Uislamu alizaliwa tarehe 17 Mfunguo Sita Rabiul Awwal mwaka huo huo. Mitazamo hiyo miwili takribani pengo lake ni kipindi cha wiki moja. Kwa kuzingatia hali hiyo, Imam Ruhullah al-Musawi al-Khomeini (MA) Mwasisi na Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akakitaja kipindi hiki cha wiki moja kuwa Wiki ya Umoja, ili Waislamu badala ya kuvutana na kuanza kukuza tofauti za tarehe za kuzaliwa Bwana Mtume SAW wakae pamoja na kujadili umuhimu wa umoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili Waislamu na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.

3927191/

captcha