IQNA

Muqawama

Wapalestina wahimizwa kukusanyika kwa wingi Al-Aqsa wakati wa Milad-un-Nabi

17:10 - September 16, 2024
Habari ID: 3479443
IQNA – Wananchi wa Palestina katika mji mtakatifu wa al-Quds (Jerusalem)wamehimizwa na makundi mbalimbali kuzuru Msikiti wa Al-Aqsa kwa wingi katika mnasaba wa Milad –un-Nabi

Tukio hili la baraka ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Siku kama ya leo miaka 1499 inayosadifiana na tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal miaka 53 kabla ya Hijria, kwa kauli ya baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu, alizaliwa Mtume Muhammad (SAW)

Kwa mnasaba huu wa Maulidi, makundi ya Palestina yamewataka Wapalestina kukusanyika katika msikiti huo mtukufu ili kukabiliana na njama za Wazayuni.

Wanasema utawala wa Israel na walowezi wa Kizayuni wameanzisha njama zisizo na kifani za kuweka hadhi mpya katika eneo hilo takatifu.

Wito huo unakuja wakati Wazayuni wakizidisha mashambulizi katika Kiwanja cha Msikiti wa Al-Aqsa chini ya ulinzi wa wanajeshi wa utawala haramu wa Israel.

Uvamizi zaidi kama huo na ukiukaji wa utakatifu wa Al-Aqsa unatarajiwa wakati wa likizo za Kiyahudi mnamo Oktoba.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas siku ya Ijumaa ilionya juu ya matokeo ya vitendo vyovyote vya Israel vinavyolenga kubadilisha utambulisho wa Msikiti wa Al-Aqsa, eneo la tatu kwa utakatifu katika Uislamu.

Taarifa hiyo imewataka Wapalestina kuzidisha vikao vyao vya kukaa katika uwanja wa Msikiti wa Al-Aqswa ili kuzima njama hizo za Wazayuni.

Hamas pia imezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu pamoja na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kubeba majukumu yao na kuchukua hatua ya kukomesha uvamizi wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na ukiukaji wa matukufu ya Kiislamu.

Kauli hiyo imekuja wakati kundi la walowezi wa Israel linaloitwa "Wanaharakati wa Milima ya Hekalu", ambalo linatetea kubomolewa Msikiti wa Al Aqsa na kujengwa hekali ya Kizayuni limesambaza video iliyotengenezwa kwa Akili Mnemba au AI inayoonyesha moto mkubwa karibu na  Qubbat al-Sakhra katika boma la Msikiti wa al-Aqsa. Taswira hiyo imeandamana na maelezo yasemayo "Tukio hilo litajiri hivi karibunii

3489914."

Habari zinazohusiana
captcha