IQNA

Maulidi

Tunisia: Maelfu washiriki sherehe za Milad un Nabii katika msikiti wa Kihistoria

15:28 - September 17, 2024
Habari ID: 3479446
IQNA - Maelfu ya watu wa mji wa Kairouan nchini Tunisia walikusanyika Jumamosi jioni kwenye Msikiti wa kihistoria wa Uqba ibn Nafi kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), sherehe ambazo ni maarufu kama Milad un Nabii au Maulidi.

Msikiti Mkuu wa Kairouan, pia unajulikana kama Msikiti wa Uqba, huwa na sherehe kubwa za Maulidi kila mwaka.

Mwaka huu, maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya Tunisia walihudhuria sherehe hizo katika  msikiti huo ambao ni miongoni mwa misikiti ya kwanza kuanzishwa na Waislamu Afrika Kaskazini.

Sherehe za Maulidi hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Rabi' al-Awwal ambapo katika nchi nyingi za Kiislamu na jamii za Waislamu duniani huandaliwa matukio na shughuli mbalimbali za kuenzi kwa mnasaba wa siku hii.

Msikiti Mkuu wa Kairouan ulioanzishwa mwaka wa 670 na jenerali wa Kiarabu Uqba ibn Nafi, ni mojawapo ya maeneo ya Kiislamu ya kale na muhimu zaidi katika ukanda wa Afrika Kaskazini. Msikiti huo umejengwa katika eneo la zaidi ya mita za mraba 9,000.

Msikiti huo umefanyiwa ukarabati kadhaa, haswa wakati wa utawala wa silsila ya Al Aghlabi katika karne ya 9, na hapa ukliweza kupata muundo wake wa sasa.

Msikiti huo uko katika orodha ya UNESCO ya turathi za dunia na unajulikana kwa umuhimu wake wa usanifu na kihistoria, unaojumuisha vipengele kutoka kwa mitindo ya kabla ya Uislamu, Kirumi, na Byzantine.

 

4236870

 
Habari zinazohusiana
captcha