Katika zama hizi za maendeleo ya kiteknolojia, juhudi za viongozi wa Kiislamu zimefungua milango ya kipekee kwa kukuza utamaduni wa Qur’ani. Hata hivyo, ubora na athari za shughuli hizi bado zinahitaji kuboreshwa ili kufikia lengo la kweli la malezi ya kiroho.
Qur’ani Tukufu, kama kitabu cha mwongozo na hazina kamili ya kiroho, ndiyo kiini cha maisha ya Mwislamu. Mtume Muhammad (SAW) daima alihimiza kusoma, kutafakari, na kuishi kwa mujibu wa Qur’ani. Hakuridhika na usomaji wa mtu binafsi pekee, bali alianzisha vikao vya Qur’ani, elimu ya pamoja, hifadhi ya aya, na tafakuri kama sehemu muhimu ya malezi ya kidini.
Leo hii, kwa msaada wa vifaa vya kisasa, programu za Qur’ani, na upanuzi wa taasisi za Kiislamu, jamii za Waislamu zimepata fursa adhimu ya kujifunza na kufundisha Qur’ani. Lakini ni lazima tathmini ya kina ifanywe ili kuhakikisha shughuli hizi zinaendana na maisha ya Mtume na hali halisi ya leo.
Mtume Muhammad (SAW) alisisitiza mambo matatu muhimu katika uwanja huu:
1. Usomaji wa Qur’ani wa kudumu – Aliona kuwa kwa kuzoea kuisoma Qur’ani mara kwa mara basi itakuwa ni rafiki bora na mwongozo wa maisha ya Mwislamu.
2. Vikao vya Qur’ani na elimu ya pamoja – Alianzisha midahalo ya Qur’ani ili kuendeleza elimu ya pamoja na kubadilishana maarifa ya kiroho. Kupitia vikao hivi, kila mshiriki alifaidika na usomaji, hifadhi, na tafakuri ya aya.
3. Kutafakari na kutekeleza mafundisho ya Qur’ani – Mtume (SAW) alisisitiza kuwa usomaji pekee bila kuelewa na kutekeleza mafundisho ya Qur’ani hautoshi. Faida ya kweli hupatikana kwa kuelewa na kuishi kwa mujibu wa Qur’ani.
Bila shaka, kuhifadhi Qur’ani ni jambo la kuhimiza. Kuhifadhi aya na sura za Qur’ani ni ibada yenye daraja kubwa, na mwenye kuhifadhi Qur’ani anapewa nafasi ya juu mbele ya Mwenyezi Mungu katika Akhera.
3494569