Akizungumza na IQNA, Fayyazbakhsh alirejelea riwaya kutoka kwa Imamu Ja‘far al-Sadiq (AS) akisema: “Uendelevu wa Qur'ani unahakikisha kuwa inabaki kuwa mpya na yenye uhai kwa kila kizazi, na kamwe haipotezi umuhimu wake.”
Alieleza kuhusu hotuba ya Mtume Muhammad (SAW) aliyoitoa wakati wa hali ya mizozo, ambapo Mtume alizungumzia zama zijazo zilizojaa mitihani. Alipoulizwa na swahaba kuhusu njia ya wokovu katika nyakati hizo, Mtume alijibu: “Mitihani ikikuzunguka kama giza la usiku, shikilia Qur'ani kwa nguvu.”
Fayyazbakhsh alifafanua kuwa kufuata Qur'ani kwa uaminifu huleta mwongozo, lakini kuipuuzia au kuweka maoni binafsi juu ya mafundisho yake hupelekea upotofu.
Aidha, alitaja usia wa mwisho wa Imamu Ali (AS), aliyewanasihi Waislamu kwa kusema: “Kuweni na tahadhari na Qur'ani, kuwani na tahadhari na Qur'ani, wala msiruhusu wengine kuwazidi katika kunufaika nayo.”
Akizungumzia upeo wa Qur'ani, alisema kuwa Kitabu hiki hakijafungwa na zama zilizopita, bali kinazungumza na asili ya mwanadamu katika kila kipindi. “Qur'ani ni maelezo ya ukweli wa mwanadamu na asili yake ya ndani. Kwa kuwa asili ya mwanadamu haibadiliki, Qur'ani ni mwongozo kwa watu wote hadi mwisho wa wakati,” alisisitiza.
Akimnukuu tena Imam al-Sadiq (AS), Fayyazbakhsh aliongeza: “Kwa nini Qur'ani, huendelea kuwa ya kisasa na yenye mwangaza? Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuiteremsha kwa ajili ya wakati mmoja au watu fulani tu. Qur'ani ni mpya katika kila zama na kwa kila jamii hadi Siku ya Kiyama.”
3494470