IQNA

Msomi wa Kiislamu ahimiza kukuzwa 'Kanuni za Dhahabu' za Qur'ani na Sunnah

17:44 - April 27, 2025
Habari ID: 3480600
IQNA – Akitoa wito wa kuendeleza kanuni za Qur'an na Sunnah, mwanazuoni mmoja wa Kiislamu amesema kuwa Qur'an na Sunnah zinahimiza uvumilivu, amani na undugu.

Hizi ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya kitaifa na ustawi, amesema Dkt. Nighat Hashmi, mwanazuoni mashuhuri wa kimataifa wa masuala ya dini. Alikuwa akitoa mhadhara ulioratibiwa na Jumuiya ya Ujenzi wa Tabia chini ya Ofisi ya Mshauri Mkuu, Chuo Kikuu cha Kilimo Faisalabad (UAF) nchini Pakistan.

Amesema kuwa, katika nyakati hizi ambapo uvumilivu umepungua na mshikamano wa kijamii kudhoofika, ni lazima kuingiza ndani ya jamii kanuni za dhahabu za Qur'an na Sunnah, ili kuhakikisha mafanikio si tu katika maisha haya, bali pia katika Akhera.

Amesisitiza umuhimu wa kuishi kwa kuzingatia maadili ya Kiislamu kama vile subira, uaminifu, unyenyekevu na undugu.Amesema, "Ni lazima tuishi kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'an Tukufu na Sunnah katika maisha yetu ya kila siku ili kufikia mafanikio ya kweli, duniani na Akhera."

Aliwahimiza washiriki kuweka mbele subira na uvumilivu hata katika nyakati ngumu. Aidha, amesisitiza kuwa vijana ni mabalozi wa Uislamu na wanabeba jukumu la kuwasilisha ujumbe wa amani na uvumilivu wa dini hii katika kila nyanja ya maisha.

3492833

Kishikizo: MAWAIDHA qurani tukufu
captcha