IQNA

Msikiti Mtakatifu wa Makka hautafunguliwa wakati wa Siku Kuu ya Idul Adha

12:08 - July 23, 2020
Habari ID: 3472991
TEHRAN (IQNA) – Wakuu wa Saudia wamesema Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al-Masjid Al-Ḥaram, hautafunguliwa wakati wa Swala wa Idul Adha mwaka huu kutokana na hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Akizungumza na waandishi habari Meja Jenerali Muhammad Al- Ahmadi, kamanda wa kikosi cha usalama katika Msikiti Mtakatifu wa Makka mipango ya awamu ya kwanza ya Ibada ya Hija imekamilika huku akisisitiza kuwa afya ya waumini inapewa kipaumbele. Amesema kuna mipango mipya ambayo imewekwa ili kudhibiti kuingia na kutoka Mahujaji katika Msikiti Mtakatifu wa Makka na kuhakikisha kuwa sheria ya kutokaribiana inatekelezwa kwa lengo la kuzuia kuenea COVID-19.

Amesema mistari maalumu imechorwa kuainisha njia ambayo kila mwenye kuhiji atatumia wakati wa kutufu Kaaba Tukufu na pia baina ya milima ya Safa na Marwaha.

Aidha amesema watakao ruhusiwa kuingia katika Msikiti wa Makka ni wale tu wenye vibali maalumu.

Meja Jenerali Al-Ahmadi amesema Msikiti Mtakatifuwa Makka utafungwa na hakuna waumini watakaoruhusiwa kuutumia katika siku ya Arafa na siku ya Idul Adha. "Uamuzi wa kuzuia kwa muda swala katika Msikiti Mtakatifu wa Makka na maenei yake ya nje utaendelea kutekelezwa. "Watu wa Makka wanatakuwa kufuturi siku ya Arafa wakiwa majumbani mwao," amesema Al-Ahmadi.

Saudia imesema asilimia 70 ya watakaotekeleza Ibada ya Hija mwaka huu ni wafanyakazi wa kigeni waishio katika ufalme huo kutoka nchi 160 na waliosalia ni raia wa Saudia.

Taarifa za awali zilisema idadi jumla ya Mahujaji mwaka huu ni takribani watu 1,000 na hatua hiyo imechukuliwa ili kuzuia maambukizi ya corona.

Hadi kufikia leo watu 258,000 wameabukizwa corona kote Saudia na waliofariki ni 2,601.

3472053

Kishikizo: Hija ، Saudia ، Makka ، Msikiti ، masjid al haram
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha