IQNA

Jinai za Israel

Hamas yawataka Wapalestina kuilinda Al-Aqsa dhidi ya uvamizi wa Israel

15:23 - December 17, 2022
Habari ID: 3476260
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiisalmu ya Palestina, Hamas, imetoa wito kwa Wapalestina kuzidisha uwepo wao katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa mjini Al Quds (Jerusalem) ili kulinda eneo takatifu dhidi ya uvamizi wa Israel na njama za kubadilisha hadhi yake.

Muhammad Hamadeh, Msemaji wa Harakati ya Ukanda wa Ghaza huko al-Quds alisema katika taarifa yake siku ya Ijumaa kwamba, utawala haramu wa Israel una nia ya kuuyahudisha mji Quds na kubadilisha hadhi ya Msikiti wa al-Aqsa, huku akiwataka vijana Wapalestina kuzuia njama za Israel.

Wakati huo huo, zaidi ya Wapalestina elfu 70 jana waliswali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa al Aqsa.

Katika siku za karibuni, msikiti wa al Aqsa umekabiliwa na hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kiyahudi ambao waliingia kwenye msikiti huo makundi kwa makundi wakiungwa mkono na kusaidiwa na wanajeshi wa utawala wa Israel. Wazayuni hao wameshadidisha chokochoko na mashambulizi dhidi ya msikiti huo mtukufu lengo likiwa ni kuandaa mazingira ya kugawanywa nyakati na maeneo ya msikiti huo. 

Ripoti ya televisheni ya  Palestine al Yaum imeeleza kuwa, Wapalestina zaidi ya elfu 70 wakazi wa Baitul Muqaddas na wa ardhi zilizoghusubiwa mwaka 1948 na wa Ukingo wa Magharibi walisali kwa adhama kubwa Swala ya Ijumaa katika msikiti huo wa al Aqsa.

Wakati Swala ya Ijumaa ilipokuwa ikiendelea, wanajeshi wa Kizayuni walikuwa wamejizatiti katika maeneo mbalimbali ya mji wa Quds  na ya kandokando ya msikiti wa al Aqsa na kuwazuia mamia ya Wapalestina wakazi wa Ukingo wa Magharibi kuingia katika mji wa Baitul Muqaddas. 

Katika upande mwingine, Sheikh Muhammad Hossein Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa alisisitiza katika hotuba ya Swala ya Ijumaa juu ya ulazima wa kuweko mshikamano miongoni mwa Wapalestina sambamba na kuhudhuria katika msikiti huo na kushiriki siku zote na daima katika eneo hilo tukufu pamoja na kukabiliana na hujuma na uvamizi wowote wa wanajeshi na walowezi wa Kiyahudi. Amesema na hapa ninamnukuu: "tunapinga uvamizi na uchokozi wowote wa Wazayuni kwenye faragha ya kibla cha kwanza na hatutavumilia hujuma zozote".

/3481708

captcha