IQNA

Teknolojia

Waziri Mkuu wa Malaysia ataka Maadili ya Kiislamu yajumuishwe katika Akili Mnemba (AI)

16:03 - November 11, 2024
Habari ID: 3479736
IQNA - Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim amedokeza umuhimu wa kuwapa vijana wa Kiislamu elimu ya Kiislamu na ujuzi wa kiteknolojia ili kufundisha maadili ya Kiislamu katika nyanja kama vile Akili Mnemba (AI).

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri siku ya Jumapili, Anwar Ibrahim aliangazia hitaji la maarifa ya kidini, pamoja na mafunzo ya teknolojia, ili kuwaongoza wanafunzi katika kuunda Akili Mnemba yenye maadili.

Waziri Mkuu pia alitangaza kuongezeka kwa misaada ya kifedha na ufadhili wa masomo kwa Wamalaysia wanaofuata Mafunzo ya Kiislamu, Tiba, na Uhandisi, kwa kuzingatia kuhimiza maendeleo ya wanafunzi katika fani hizi.

Zaidi ya hayo, wanafunzi kutoka Maahad Tahfiz, taasisi ambazo kijadi huzingatia masomo ya Qur'ani, sasa wanahimizwa kuchunguza programu za Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET).

Anwar alibainisha kuwa hii inawaruhusu kujifunza uhandisi, AI, na ujuzi mwingine huku wakidumisha ustadi wao katika Qur'ani na Kiarabu. Wengine wamefaulu hata kuwa marubani” aliongeza, akisisitiza nafasi nyingi za kazi kwa wanafunzi hao.

3490642

Habari zinazohusiana
Kishikizo: malaysia teknolojia
captcha