IQNA

Mashindano ya 26 ya Qur’ani ya Sheikha Hind bint Maktoum Yakamilika

16:27 - December 13, 2025
Habari ID: 3481654
IQNA- Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai (DIHQA) imetangaza kukamilika kwa Mashindano ya 26 ya Qur’ani ya Sheikha Hind bint Maktoum.

Kwa mujibu wa DIHQA, mashindano ya mwaka huu yalishuhudia mahudhurio makubwa na idadi isiyowahi kutokea ya washiriki, jambo linaloonyesha hadhi ya tuzo hiyo na mchango wake unaozidi kuongezeka katika kuhudumia Qur’ani Tukufu, pamoja na kukuza utamaduni wa kuhifadhi na kuimudu miongoni mwa jamii ya Wamuungano wa Falme za Kiarabu na wakazi wake.

Jumla ya washiriki katika toleo hili ilifikia washiriki 1,666 wa kiume na wa kike kutoka makundi na umri tofauti, wanaume 868 na wanawake 798, ikiwa ni ishara ya upana na utofauti wa ushiriki.

Washiriki walitoka katika mataifa 55 ya Kiarabu, Asia, Afrika na Ulaya. Raia wa Umoja wa Falme za Kiarabu waliongoza kwa idadi kubwa zaidi, wakifikia washiriki 1,028, kiwango cha juu zaidi cha ushiriki wa raia katika historia ya mashindano haya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Tuzo hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mambo ya Kiislamu na Shughuli za Kijamii Dubai, Ahmed Darwish Al Muhairi, alisema kuwa mashindano haya yamekuwa jukwaa muhimu la kuvutia mahafidh bora wa Qur’ani kutoka mataifa mbalimbali wanaoishi nchini humo. Aliongeza kuwa ongezeko la ushiriki linaonyesha dhamira ya serikali kuunga mkono miradi ya Qur’ani inayolenga kulea kizazi kinachofahamu vyema Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Washindi na waliofuzu hatua za mwisho wanatarajiwa kuheshimiwa katika hafla maalumu itakayofanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ujao, chini ya udhamini wa Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Waziri Mkuu wa UAE na Mtawala wa Dubai.

3495710

Habari zinazohusiana
captcha