IQNA

Ilhan Omar: Kwa kunishambulia, Trump anajaribu kugeuza macho ya umma kutoka kwenye kashfa ya Epstein

11:23 - February 13, 2026
Habari ID: 3481928
IQNA-Ilhan Omar mwakilishi Mwislamu wa Bunge la Marekani, akijibu tuhuma za Donald Trump dhidi yake, alimtaja Trump kama mnyanyasaji kingono wa watoto, akisema kuwa tuhuma anazotoa mtawala huo wa Marekani dhidi yake ni jaribio la kugeuza mawazo ya umma kutoka kwenye kashfa ya Jeffrey Epstein.

Mvutano kati ya Trump na Ilhan Omar, mbunge wa jimbo la Minnesota, umeongezeka baada ya Trump kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya jamii ya Wasomali katika jimbo hilo, akimwita Omar kuwa “mwawakilishi bandia wa Bunge” na kuwatuhumu wakimbizi wa Kisomali kwa kusababisha hasara za kiuchumi na kile alichokiita “kupenya” katika jamii ya Marekani.

Kauli hizi zilitolewa wakati wa mahojiano ya Trump na Fox Business, akizungumza na Larry Kudlow, ambapo alijadili hali ya Minnesota na kuituhumu moja kwa moja jamii ya Wasomali, akidai kuwa uwepo wao umeathiri vibaya jimbo hilo.

Katika mahojiano hayo, Trump alisema kuwa wakimbizi wamesababisha hasara kubwa, na akaongeza:

“Wasomali wamefurika hapa. Unaona walichofanya kwa nchi yetu. Wamepenya katika nchi yetu, na wana yule mwakilishi bandia wa Bunge (Ilhan Omar). Wanachofanya ni kibaya sana.”

Trump pia alidai kuwa jimbo la Minnesota limekumbwa na kile alichokiita “ufisadi wa dola bilioni 19" hasa katika sekta kama huduma za afya, na akaahidi kuwa utawala wake unajitahidi kufichua mizizi ya kesi hizo na ukweli wake.

Kwa upande wake, Ilhan Omar, mwanasiasa wa chama cha Democratic mwenye asili ya Kisomali, alijibu kauli za Trump kupitia mitandao ya kijamii. Alishiriki kipande cha mahojiano hayo na kuongeza tamko kali lililorejea moja kwa moja kwenye kesi ya Jeffrey Epstein, anayeshtakiwa kwa kuendesha mtandao wa unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto na biashara haramu ya binadamu.

Omar aliandika:

“Kiongozi wa ‘chama cha kuwanyayasa watot kingono’ anajaribu kuficha ukweli kwamba jina lake linatajwa katika kila faili ya Epstein. Angalau Somalia, wanyanyasaji wa watoto hawachaguliwi bali wananyongwa.”

Habari inayohusiana:

Kauli ya Omar imegusa moja ya masuala nyeti zaidi ambayo yamekuwa yakimwandama Trump katika maisha yake ya kisiasa: uhusiano wake wa zamani na Epstein, kesi ambayo imezua mjadala na hasira kubwa si tu Marekani bali pia kimataifa.

Kwa mujibu wa wakosoaji wa Trump, nyaraka zilizotolewa na Idara ya Sheria ya Marekani kama sehemu ya kesi ya Epstein zinataja jina la Trump “maelfu ya mara”. Hata hivyo, ripoti hiyo hiyo, iliyoandaliwa chini ya maafisa wa utawala wa Trump, inaonyesha kuwa bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha kuhusika kwake au hatia ya kisheria, madai ambayo wabunge wengi wanayaangalia kwa shaka.

Ilhan Omar anaamini kuwa mashambulizi ya mara kwa mara ya Trump dhidi ya Wasomali, na juhudi zake za kuwasilisha kama tishio la ndani, ni sehemu ya mkakati mpana wa kile anachokiita “kufunika” kashfa mpya inayohusiana na uhusiano wake wa zamani na Epstein.

4334126

 

Habari zinazohusiana
captcha