IQNA

Swala na Qur'ani Humpa Amad Diallo wa Manchester United Nguvu na Utulivu wa Kipekee

15:33 - February 20, 2026
Habari ID: 3481962
IQNA – Wakati ustadi wake wa kuchezesha mpira unawatia mshangao mabeki uwanjani, Amad Diallowinga wa timu ya Ligi Kuu ya Uingereza, EPL, Manchester United anabainisha kuwa chanzo chake cha kweli cha nguvu na uthabiti kinatokana na imani yake.

Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast, anayekipiga katika klabu ya England Manchester United, amezungumzia kwa uwazi upande wa kidini wa maisha yake, akisisitiza kuwa anajitahidi kudumisha swala za kila siku na kusikiliza Qur’ani Tukufu mara kwa mara.

Akizungumza katika mahojiano na chaneli rasmi ya klabu, Diallo alielezea ratiba yake ya asubuhi kwa kusema:

“Huamka mapema sana na kufanya mazoezi ya kunyoosha mwili nyumbani. Huanzia siku yangu kwa swala kwanza, kisha ninapofika Carrington nakula chakula chepesi,” alifafanua.

Aliendelea kueleza maandalizi yake ya lishe kabla ya mechi:

“Iwapo tunacheza mechi ya mapema, kama saa sita mchana, hula kifungua kinywa. Na kama mechi ni saa nane mchana, hula chakula kidogo cha mchana,” aliongeza.

Mshambuliaji huyo kijana pia alifichua desturi yake kabla ya kuingia uwanjani:

Habari inayohusiana:

“Kabla ya mechi napenda kusikiliza Qur’ani Tukufu, kwa sababu hunipa nguvu kubwa na huniletea utulivu wa moyo. Hili lina uhusiano wa moja kwa moja na dini. Wakati mwingine nasikiliza muziki, lakini mara nyingi napendelea kusikiliza Qur’ani,” alihitimisha.

3496471

captcha