IQNA

Fainali za Mashindano ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani ya “Mafaza”

15:22 - June 01, 2026
Habari ID: 3482312
IQNA – Raundi ya fainali ya Mashindano ya Qur’ani yanayorushwa mubashara kupitia televisheni, “Inna lil-Muttaqina Mafaza” (Hakika kwa wachamungu ipo mafanikio/maokoleo), inatarajiwa kufanyika baadaye wiki hii.

Mtandao wa Televisheni ya Al-Kawthar utafanya fainali ya mashindano hayo mubashara usiku wa kuamkia ‘Eid ul Ghadir (Jumatano, Juni 3), kwa mujibu wa Ofisi ya Mahusiano ya Umma ya mtandao huo.

Mashindano hayo, ambayo yalikuwa yakirushwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, yalikatishwa kufuatia vita vya kikatili” vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vilivyoanza tarehe 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani sawa na tarehe 28 Februari.

Wakati huo, “maadui wa Uislamu”, huki wakikiuka viwango na sheria za kimataifa, walilenga maeneo ya raia, yakiwemo baadhi ya majengo ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), ambalo linamiliki Al-Kawthar TV, jambo lililosababisha kusitishwa kwa matangazo ya programu hii ya Qur’ani.

Mtandao wa Al-Kawthar, huku ukithamini uungaji mkono wa watazamaji na washiriki wa msimu huu, uliomba radhi kwa kusitishwa huko kwa wapenzi wote wa Qur’ani Tukufu, hasa wale waliofanikiwa kufika hatua ya fainali, na ukaeleza matumaini yake kwamba, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Umma wa Kiislamu utashuhudia ushindi wa maamuzi dhidi ya maadui wa Uislamu na “ukombozi kamili wa ardhi za Kiislamu”.

Kwa mujibu wa waandaaji, baada ya kutathmini matokeo ya washiriki katika usiku kumi za mwanzo za mwezi mtukufu wa Ramadhani, wasomaji watano bora kutoka nchi tano tofauti, waliopata alama za juu zaidi, wamechaguliwa kushiriki hatua ya fainali. Wasomaji hao watasoma na kushindana mubashara kwenye shindano la televisheni ili kuwania taji la juu la toleo la 19.

Mashindano ya Qur’ani ya kupiga simu (phone-in) yenye jina “Inna lil-Muttaqina Mafaza” (Hakika kwa wachamungu ipo mafanikio—Qur’ani Tukufu, 78:31) yanatajwa kuwa mashindano ya kwanza duniani ya kisomo cha Qur’ani kupitia televisheni.

Kwa miaka 19 hadi sasa, yamekuwa yakirushwa mubashara kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ni miongoni mwa mashindano makubwa zaidi ya mubashara ya kisomo cha Qur’ani katika ulimwengu wa Kiislamu, yakitangazwa na Al-Kawthar—kituo cha Kiarabu kilicho chini ya Kitengo cha Kimataifa cha IRIB.

Katika miaka iliyopita, mashindano hayo yamekuwa jukwaa la kuibua na kutambulisha vipaji bora vya Qur’ani kutoka nchi mbalimbali, na daima yamepokelewa kwa mapokezi makubwa na maashiki wa Qur'ani Tukufu.

3497670

Habari zinazohusiana
captcha