IQNA

Chuo kipya cha Qur’ani chazinduliwa Yemen

17:29 - July 14, 2026
Habari ID: 3482487
IQNA – Chuo Kikuu cha Qur’ani na Shule ya Mafunzo ya Kidini cha Juu kimefunguliwa katika mji wa Rida, mkoani Bayda, nchini Yemen, Jumapili.

Chuo hiki na shule ya masomo ya kidini, ambayo ni tawi la Chuo cha Qur’ani Tukufu cha Yemen, kilizinduliwa katika Msikiti wa Ammar bin Yasser uliopo wilayani Wald Rabi’, na hafla ya ufunguzi ilifanyika sambamba na kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Zayd bin Ali (AS), kwa mujibu wa tovuti ya Al-Thawra.

Katika hafla hiyo, iliyohudhuriwa na naibu magavana wa mkoa huo, Abdul Salam Al-Nusiri na Nasser Al-Aji, umuhimu wa taasisi hii mpya ya elimu katika kuitumikia Qur’ani na kufundisha sayansi za Qur’ani ulisisitizwa.

Wazungumzaji pia walisema kuwa vituo hivi vina mchango mkubwa katika kuwalea na kuwafunza wanazuoni mashuhuri wa dini na wahubiri nchini Yemen, na kwamba hatua kama hizi zitasaidia kupanua uelewa wa kidini na kukuza maadili ya Kiislamu katika ngazi ya jamii.

Wakasisitiza kuwa uzinduzi wa chuo na shule hii unaonesha dhamira ya dhati kwa elimu ya Qur’ani na ya kidini, pamoja na juhudi za kujifunza kutokana na maadili yaliyohimizwa na Zayd ibn Ali (AS), hasa katika kushikamana na Qur’ani na misingi ya Kiislamu.

Washiriki, wakithamini juhudi za waliohusika na waliounga mkono mradi huu wa kielimu, walisisitiza nafasi yake muhimu katika kulea vizazi vyenye elimu ya dini na manufaa, vinavyoweza kulitumikia jamii.

Sherehe hiyo ilijumuisha vipengele mbalimbali vilivyofafanua hadhi ya Qur’ani na nafasi yake katika kumjenga mtu binafsi na jamii.

Zayd bin Ali bin Al-Hussein (AS), mwana wa Imam Sajjad (A.S.), ni miongoni mwa watu mashuhuri katika Uislamu wa Kishia na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla. Ameelezwa kuwa ni “Halif al-Qur’an” yaani mshirika na mtekelezaji wa Qur’ani, kutokana na uelewa wake mkubwa wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Mnamo mwaka 121 Hijria Qamaria, Zayd bin Ali alimuasi Khalifa wa Bani Umayya, Hisham ibn Abdul Malik, na kundi la watu likatangaza kumtii. Aliuawa shahidi katika vita vilivyotokea mjini Kufa kati yake na jeshi la khalifa huyo dhalimu.

3498237

Habari zinazohusiana
Kishikizo: yemen qurani tukufu
captcha