IQNA

Muqawama

Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen asisitiza ulazima wa kuiga mfano wa Mtume Mtukufu (SAW).

11:42 - September 06, 2024
Habari ID: 3479387
IQNA- Badreddin Abdul Malik al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, katika hotuba yake kuhusu hali mbaya ya hivi sasa ya Umma wa Kiislamu amesema kuna ulazima kufungamana na Mtume Muhammad (SAW0 Mtume na Qur'ani Tukufu, amesisitiza haja ya Waislamu kusoma na kuiga shakhsia ya Mtume (SAW).

Kiongozi wa Ansarullah amesema katika hotuba yake siku ya Alkhamisi akiwa katika mji mkuu wa Yemen, San'aa kwamba: Waislamu wanapaswa kuchunguza shakhsia ya Mtukufu Mtume (SAW) na kuiga mfano wake. Umma wa Kiislamu leo unatakiwa urejee kwenye mwenendo na Sunnah za Mtume leo. Udhaifu wa uhusiano uliopo baina ya Umma wa Kiislamu na Mtume (SAW) na Qur'ani umesababisha leo hii kuangukia katika matatizo yaliyopo na kuandaa mazingira ya maovu ya maadui.

Al Houthi pia amezikosoa baadhi ya tawala za Kiarabu kwa kukaa kimya huku utawala ghasibu wa Israel ukiendelea na ukatili wake dhidi ya Wapalestina na kukivunjia heshima kitabu kitukufu cha Kiislamu cha Qur'ani katika Ukanda wa Gaza.

Ameongeza kuwa: "Nchi za Kiarabu zinatazama tu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, mashambulizi ya kuchomwa moto misikiti na kuvunjiwa heshima nakala za Qur'ani Tukufu bila ya kuwa na misimamo ya wazi kuhusiana na suala hilo."

Al-Houthi amesisitiza umuhimu wa wote katika ulimwengu wa Kiislamu kuwa na roho ya kujitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, yaani Jihadi, huku akionya kwamba Waislamu watapoteza heshima na uhuru wao ikiwa watapuuza suala hilo muhimu.

Kiongozi huyo wa Ansarullah ameendelea kusema kuwa: "Baadhi ya tawala za nchi za Kiarabu zinajaribu kumtuliza adui Mzayuni na kufikia mapatano naye ili kujilinda". Ameziona tawala hizo za Kiarabu kwamba hataka kama zitajipendekeza kwa adui, hatimaye zitatupiliwa mbali pindi zitakapokuwa hazitakiwi tena.

Mkuu wa Ansarullah ameendelea kuwapongeza wapiganaji wa muqawama wa Palestina walioko Gaza kwa kupambana na vikosi vya kijeshi vya Israel kwa silaha zisizo za kisasa na kusema: “Hata majeshi makubwa ya baadhi ya nchi za Kiarabu hayakuweza kustahimili mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni kwa kiasi kikubwa kama walivyofanya wapiganaji wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Amesisitiza kuwa wananchi wa Gaza wanastahimili mashambulizi ya kikatili ya Israel na vita vya mauaji ya halaiki, ambavyo vimeamsha dhamiri ya binadamu hata katika nchi zisizo za Kiislamu.

Kwingineko katika matamshi yake, Kiongozi wa Ansarullah ameashiria operesheni za kijeshi za baharini za Yemen dhidi ya meli za kibiashara zenye mafungamano na utawala haramu wa Israel na kusema operesheni hizo zinafanyika kuwaunga mkono Wapalestina wa Ukanda wa Gaza. Amesisitiza kuwa, maadui wamekiri kushindwa kwao kusimamisha operesheni hizo za kijeshi za kulipiza kisasi katika Bahari Nyekundu na nje ya Bahari Nyekundu.

 4235117

Habari zinazohusiana
captcha