iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)-Mtu moja aliyemsikia mwanachama wa chama chenye chuki dhidi ya Uislamu akiwataka watu waisome Qur'ani kwa lengo la kuikosoa alifuata ushauri huo lakini kinyume na ilivyotarajiwa, alipata muongozo na kusilimu.
Habari ID: 3471204    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/10/04

TEHRAN (IQNA)-Mahakama moja nchini Saudi Arabia imesema Shirika la Ujenzi la Binladin halina hatia na haliwezi kubebeshwa dhima ya kuanguka winchi (crane) katika Msikiti Mtakatifu wa Makka wakati wa msimu wa Hija mwaka 2015.
Habari ID: 3471203    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/10/03

TEHRAN (IQNA)- Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) limechukua uamzui wa kihistoria wa kuondoa marufuku ya muda mrefu ya wanawake Waislamu kuvaa Hijabu wanapocheza.
Habari ID: 3471202    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/10/03

TEHRAN (IQNA)-Bunge la Ufilipino limepitisha muswada wa sheria ya kutangaza tarehe mosi Februari kila mwaka kuwa Siku ya Kitaifa ya Hijabu nchini humo.
Habari ID: 3471201    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/10/02

TEHRAN (IQNA) Siku ya leo inasadifiana na mwezi 10 Muharram 1439 Hijria, siku ya kukumbuka wakati damu ilipoushinda upanga kwa ushujaa wa Imam Hussein AS na wafuasi wake wachache katika jangwa la Karbla la Iraq ya leo.
Habari ID: 3471200    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/10/01

TEHRAN (IQNA)- Waislamu wa madhehebu ya Shia kote duniani wanashiriki katika maadhimisho ya Siku ya Tasu'a, wakifanya maombelezo ya kukumbuka mapambano ya Karbala yaliyopelekea kuuawa shahidi Imam Hussein AS.
Habari ID: 3471199    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/30

TEHRAN (IQNA)-Msichana mwenye umri wa miaka 10 ataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Shaikha Fatima Bint Mubarak ya Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE.
Habari ID: 3471198    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/29

TEHRAN (IQNA)-Polisi katika mkoa wa Xinjiang kaskazini magharibi mwa China wameamuru familia za Waislamu kukabidhi madhihirisho ya kidini hasa nakala za Qur'ani na misala.
Habari ID: 3471197    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/28

TEHRAN (IQNA)-Mtafiti mmoja nchini Misri amesema mkataba aliofunga Bwana Mtume Muhammad SAW na Wakristo ni hati ya kwanza kuhusiana na kuheshimu dini tofauti duniani.
Habari ID: 3471196    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/28

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amekwenda katika Msikiti wa Imam Husain AS hapa Tehran na kuusomea Faatiha mwili mtoharifu wa shahid Mohsen Hojaji, aliyeuliwa shahidi na magaidi wa Daesh au ISIS wakati akilinda Haram ya mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW, Bibi Zaynab al Kubra AS nchini Syria.
Habari ID: 3471195    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/27

TEHRAN (IQNA)-Msikiti umeteketezwa moto katika mji wa Orebro kusini mwa Sweden katika tukio ambalo linaaminika kutekelezwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3471194    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/26

TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu Misri Sheikh Mohamed Mokhtar Gomaa amesema wizara yake itaanzisha shule za Qur’ani katika misikiti yote mikubwa nchini humo.
Habari ID: 3471193    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/26

TEHRAN (IQNA)- Waislamu wanajumuika katika Msikiti wa Al Ghadir mjini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ajili ya maombolezo ya kuuawa Imam Hussein AS katika mwezi wa Muharram.
Habari ID: 3471192    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/26

TEHRAN (IQNA)-Watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wamemdunga kisu na kumjeruhi daktari Muislamu katika mji wa Manchester nchini Uingereza.
Habari ID: 3471191    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/25

Imam Hussein AS alisema: Mja ambaye atamuabudu Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki kuabudiwa, Mwenyezi atampa kilicho zaidi ya alichokiomba. (Mawsuat Kalimat al-Imam al-Hussein AS. Hadithi ya 906, Uk. 748)
Habari ID: 3471190    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/25

TEHRAN (IQNA) Jumuiya ya Kiislamu ya Maelewano ya Kitaifa ya Bahrain (Al Wefaq) imelaani hatua ya vikosi vya usalama kuhujumu madhihirisho ya Ashura na kuendelea kuzingirwa nyumba ya mwanazuoni wa Kiislamu Sheikh Issa Qassim.
Habari ID: 3471189    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/24

Msomi wa Ahul Sunna nchini Lebanon
TEHRAN (IQNA)-Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Ahlul Sunna nchini Lebanon amesema mwamko wa Imam Hussein AS dhidi ya utawala wa kiimla na kidhalimu wa Yazid.
Habari ID: 3471188    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/23

Amnesty International
TEHRAN (IQNA)-Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International wamesema kuwa, bomu lililoua raia 16 wa Yemen wakiwemo watu wote wa familia ya mtoto Buthaina aliyenusurika shambulizi hilo, lilitengenezwa nchini Marekani.
Habari ID: 3471187    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/23

TEHRAN (IQNA)-Waislamu barani Ulaya wanahisi kuongezeka ubaguzi ambapo wawili kati ya watano (asilimia 40) wakisema wamekumbana na ubaguzi wakati wa kutafuta kazi, nyumba au huduma za umma kama vile elimu an matibabu.
Habari ID: 3471186    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/22

Katika Hotuba Umoja wa Mataifa
TEHRAN (IQNA)-Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amehutubu katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuitahadharisha Marekani kuhusu hatua yoyote ya kukiuka mapatano ya nyuklia ya Iran.
Habari ID: 3471185    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/21