TEHRAN (IQNA) – Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, ambaye yuko New York kuhudhuria mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3472145 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/23
TEHRAN (IQNA) – Misikiti 44 kote Afrika Kusini itafungua milango wazi kwa umma mnamo Septemba 24 katika Siku ya Turathi, ambayo lengo lake ni kuleta maelewano ya kijamii na kuunda taifa lenye kuwajumuisha wote katika nchi hiyo.
Habari ID: 3472140 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/20
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu maalumu kwa watu wenye ulemavu wa macho kimefunguliwa nchini Russia katika eneo la Dagestan mapema wiki hii.
Habari ID: 3472138 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/19
TEHRAN (IQNA) Waislamu wasiopungua laki sita wa jamii ya Rohingya waliosalia nchini Myanmar wangali wanakabiliwa na hatari kubwa ya kuuliwa kwa kimbari.
Habari ID: 3472136 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/18
TEHRAN (IQNA) – Shirika moja la kutetea haki a binadamu limeitaka serikali ya China kuwaachilia huru watoto Waislamu wa jamii ya Uighur wanaoshikiliwa kinyume cha matakwa ya wazazi wao katika shule za bweni za serikali mkoani Xinjiang.
Habari ID: 3472132 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/16
TEHRAN (IQNA) – Meya Mwislamu huko New Jersey nchini Marekani amesema alishikiliwa kwa muda katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa John F. Kennedy mjini New York mwezi uliopita ambapo maafisa wa usalama walimsaili kuhusu iwapo anawafahamu magaidi.
Habari ID: 3472129 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/14
Khatibu wa Swala ya Ijumaa
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria mapambano ya Kiislamu (muqawama) na kusimama kidete wananchi wa Syria, Lebanon, Iraq, Bahrain na Yemen mbele ya mabebebu na waistikabari na kusisitiza kuwa, somo la Ashura na harakati ya Imam Hussein AS ni chimbuko la muqawama wa wananchi wa eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).
Habari ID: 3472128 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/13
TEHRAN (IQNA) – Waalimu wametimuliwa katika shule moja huko Montreal, Canada baada ya kusistiza kuendelea kuva vazi la staha la Kiislamu, Hijab.
Habari ID: 3472127 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/12
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa kidini nchini Saudi Arabia amekamatwa baada ya kukosoa sera za ufalme za kuwakaribisha watumbuizaji wa kimataifa wanaoeneza ufasiki na ufisadi wa kimaadili.
Habari ID: 3472126 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/11
TEHRAN (IQNA) - Mamilioni ya Waislamu kote duniani hii leo wanaomboleza katika siku ya Ashura ambayo ni siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS.
Habari ID: 3472122 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/10
TEHRAN (IQNA) – Waislamu kote duniani usiku wa kuamkia leo tarehe 9 Mfunguo Nne Muharram wameshiriki katika vikao, majlisi na shughuli za maombolezo na kukumbuka misiba na masaibu yaliyomkuta mjukuu wa Mtume wetu Muhammad SAW, Imam Hussein bin Ali AS, ndugu na mswahaba zake waaminifu huko Karbala nchini Iraq mwaka 61 Hijria.
Habari ID: 3472121 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/09
TEHRAN (IQNA) – India imeweka sheria ya kutotoka nje katika sehemu kadhaa la eneo linalozozaniwa la Kashmir baada ya jeshi kkuwashambulia Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa wanashiriki katika maombolezo ya mwezi wa Muharram.
Habari ID: 3472120 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/08
TEHRAN (IQNA) - Utawala wa kiimla wa Bahrain umeanzisha wimbi jipya la kuwakandamiza wanazuoni wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia katika mwezi huu wa Muharram.
Habari ID: 3472118 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/07
TEHRAN (IQNA) - Mijumuiko ya Kimataifa kwa jina la "Watoto Wachanga Wanaonyonya wa Hussein AS" imefanyika leo Ijumaa katika zaidi ya maeneo elfu sita katika Iran ya Kiislamu na katika nchi 45 duniani sambamba na Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram.
Habari ID: 3472117 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/06
TEHRAN (IQNA)- Mzungu mbaguzi mwenye kufuatia itikadi ya wale wanaoamini wazungu ndio wanadamu bora zaidi duniani, amefungwa jela miaka 12 nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kuchochea mauaji ya Waislamu.
Habari ID: 3472114 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/04
TEHRAN (IQNA) - Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amemuandikia barua Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kushukuru yale aliyoyazungumza katika mkutano wake na ujumbe wa harakati hiyo uliofanya ziara hapa mjini Tehran hivi karibuni .
Habari ID: 3472110 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/02
TEHRAN (IQNA) – Vijana kadhaa waliohifadhi Qur'ani Tukufu nchini Bulgaria wameenziwa na kutunukiwa zawadi.
Habari ID: 3472106 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/30
Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
TEHRAN (IQNA) – Yahya (Christian) Bonaud, mwanafikra Mfaransa, msomi na mtarjumi wa Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa amefariki Jumatatu akiwa na umri wa miaka 62.
Habari ID: 3472103 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/27
TEHRAN (IQNA) - Wakimbizi wapatao laki mbili Waislamu wa jamii ya Rohingya wa nchini Myanmar Jumapili walishiriki kwenye kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu jeshi la Myanmar lilipowakandamiza na kuwalazimisha kuyahama makazi yao kwa umati na kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh ili kunusuru maisha yao.
Habari ID: 3472102 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/27
TEHRAN (IQNA) – Mcheza soka mstaafu wa kulipwa barani Ulaya, Frederic Oumar Kanoute, mwenye asili ya Afrika anaongoza mkakati wa kujenga msikiti huko Sevilla nchini Uhispania.
Habari ID: 3472096 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/23