waislamu - Ukurasa 53

IQNA

TEHRAN (IQNA) - Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) zimepinga mpango wa 'muamala wa karne' uliopendekezwa na Marekani ambao unakandamiza haki za taifa la Palestina.
Habari ID: 3472435   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/03

TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja 'Muamala wa Karne' kama mpango wa Marekani wa kufedhehesha, aibu na wenye kuchukiza.
Habari ID: 3472432   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/02

TEHRAN (IQNA) – Msomi nchini Afrika Kusini amesema jamii barani Afrika zina nafasi muhimu katika kukabiliana na misimamo mikali ya kidini kwani serikali pekee haziwezi kukabiliana na tatizo hilo.
Habari ID: 3472431   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/02

TEHRAN (IQNA) – Iwapo Waislamu nchini Marekani wanataka 'kuonekana' na masuala yao yazingatiwe katika ngazi za maamuzi muhimu, basi wanapaswa kushiriki katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo.
Habari ID: 3472430   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/01

Khatibu wa Sala ya Ijuma Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameilaani Marekani kwa kuanzisha njama mpya dhidi ya Waislamu kwa jina la "Muamala wa Karne" na kusema kuwa, njama hizo zitafeli na kushindwa tu.
Habari ID: 3472425   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/31

TEHRAN (IQNA) - Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo na kuwajeruhi Wapalestina kadhaa waliokuwa wamefika hapo kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3472423   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/31

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pendekezo la Marekani lililopewa jina la 'Muamala wa Karne' katu halitazaa matunda kwa Rehema za Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3472421   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/30

TEHRAN (IQNA) – Kauli mbiu ya Maonyesho ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran itakuwa ni 'Qur'ani Tukufu Kitabu cha Ustawi."
Habari ID: 3472420   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/30

Katika barua maalumu
TEHRAN (IQNA) - Spika wa Bunge la Iran (Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu) ametoa wito wa kukabiliana na mpango bandia wa Rais Donald Trump uliopewa jina la "Muamala wa Karne". Aidha ametoa wito kutatuliwa mgogoro wa Palestina kwa kutumia njia ya kura ya maoni na udiplomasia wa kibunge.
Habari ID: 3472418   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/29

TEHRAN (IQNA)- Leo ni Jumatano tarehe Tatu Jamadithani 1441 Hijria sawa na 29 Januari 2020. Siku kama ya leo, miaka 1430 iliyopita, sawa na tarehe tatu Jamadithani mwaka wa 11 Hijiria alikufa shahidi Bibi Fatimatu Zahra SA, binti wa Mtume Muhammad SAW na mke wa Imam Ali Bin Abi Twalib AS.
Habari ID: 3472415   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/29

TEHRAN (IQNA) – Rais wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina amezitaka nchi za Kiislamu na Kiarabu kususia uzinduzi wa mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na mgogoro wa Palestina uliopewa jina la "Muamala wa Karne".
Habari ID: 3472412   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/28

TEHRAN (IQNA) – Shirika la Ndege la Delta Airlines la Marekani limetozwa faini ya dola 50,000 kwa kuwatimua wasafiri watatu Waislamu ambao tayari walikuwa wameshapanda ndege hata baada ya maafisa wa usalama kusema hakukuwa na tatizo lolote la usalama.
Habari ID: 3472407   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/26

TEHRAN (IQNA) - Brigedi za Hizbullah ya Iraq zimesema kuwa mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo yataendelea hadi wavamizi wote wa Kimarekani watakapofurushwa kikamilifu nchini Iraq na katika eneo zima la Asia Magharibi.
Habari ID: 3472405   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/25

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi-Fard
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa mauaji yaliyofanywa na jeshi la kigaidi la Marekani dhidi ya Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni mwanzo wa kufukuzwa Marekani katika eneo hili la magharibi mwa Asia sambamba na washirika wake katika eneo kusambaratika.
Habari ID: 3472403   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/24

TEHRAN (IQNA) – Watu wa matabaka mbali mbali nchini Afrika Kusini wamekusanyika mbele ya Ubalozi wa Marekani mjini Pretoria kulaani sera za Rais Trump wa Marekani dhidi ya Iran.
Habari ID: 3472400   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/23

TEHRAN (IQNA) – Baraza la Shura (Mashauriano) la Jumuiya ya Waislamu Uingereza limemchagua Bi. Raghad Al Tikriti kuwa mwenyekiti wake mpya.
Habari ID: 3472398   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/23

TEHRAN (IQNA) - Wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi kwa kuwapiga risasi Wapalestina watatu katika uzio wa Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3472396   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/22

TEHRAN (IQNA) – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limeanzisha kampeni maalumu ya kuwahimiza Waislamu kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa rais utakaofanyika nchini humo mwaka 2020.
Habari ID: 3472395   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/22

TEHRAN (IQNA) – Awamu ya kwanza ya ukarabati muhimu wa Msikiti wa Al Nouri mjini Mosul Iraq imekamilika. Msikiti huo ulihujumiwa na kubomolewa na kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) mwaka 2017.
Habari ID: 3472394   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/22

TEHRAN (IQNA)- Misri imeandaa hafla ya kumbukumbu ya kuzaliwa qarii mashuhuri wa Qur'ani Tukufu nchini humo Mohamed Siddiq El-Minshawi.
Habari ID: 3472392   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/21