iqna

IQNA

Ustadh Ahmed Ahmed Nuaina
Qarii mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kutoka Misri amesema mafundisho ya Qur’ani yanapaswa kutekelezwa katika sekta zote za maisha.
Habari ID: 3470527    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/17

Mshukiwa mmoja amefikishwa mahakamani Marekani baada ya kubainika kuwa alimpiga risasi na kumua Imamu wa msikiti na Mwislamu aliyekuwa naye huko mjini New York huku Waislamu wakitaka uadilifu na haki.
Habari ID: 3470526    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/17

Mgahawa Halali ulio katika makao ya wanariadha katika michezo ya Olimpiki huko Rio de Janeiro nchini Brazil mbali na kuwavutia wanariadha Waislamu pia unawavutia wasiokuwa Waislamu.
Habari ID: 3470524    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/15

Imam wa msikiti mmoja katika jimbo la New York nchini Marekani ameuawa kwa kufyatuliwa risasi katika hujuma ya kigaidi.
Habari ID: 3470522    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/14

Sayyid Hassan Nasrullah
Kiongozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameyataka makundi ya kigaidi na kitakfiri kuweka chini silaha na yatambue kuwa harakati zao hazina maslahi kwa yeyote isipokuwa adui Marekani.
Habari ID: 3470521    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/14

Tarehe 11 Mfunguo Pili Dhil Qaada ni siku ya maadhimisho ya kuzaliwa Imam Ali bin Musa ar-Ridha AS, mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW.
Habari ID: 3470520    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/14

Shirika moja la kutetea haki za binadamu Nigeria limetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwafikisha kizimbani wanajeshi waliohusika katika kuwaua Waislamu wa madhehebu ya Shia mwezi Desemba mwaka jana.
Habari ID: 3470516    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/11

Mwandishi mwenye asili ya Somalia amebaini kuwa vyombo vya habari vya Magharibi hupuuza na kutozingaita habari kuhusu Waislamu wanaouawa katika vitendo vya kigaidi hasa nchini Somalia.
Habari ID: 3470515    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/11

Wanafunzi Wakristo nchini Zimbabwe wameshiriki katika warsha ya siku moja kuhusu Uislamu.
Habari ID: 3470510    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/09

Duka moja la bidhaa halali nchini Ufaransa limeonywa kuwa iwapo haliafiki kuuza pombe na nyama ya nguruwe basi litapokonywa leseni na kufungwa.
Habari ID: 3470507    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/08

Kituo cha utamaduni cha Iran nchini Senegal kimeandaa warsha kuhusu kusoma Qur’ani kwa tajwid katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.
Habari ID: 3470506    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/08

Mwanamke Mwislamu nchini Marekani amefutwa kazi baada kutokana na kuvaa vazi la Hijabu akiwa kazini.
Habari ID: 3470501    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/07

Kozi ya mafunzo ya Kiislamu katika kipindi cha muda mfupi imemamalizika hivi karibuni nchini Uganda kwa kutolewa zawadi kwa wanafunzi bora.
Habari ID: 3470500    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/07

Michezo ya Olimpiki mwaka 2016 imeanza Jumamosi katika mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil huku wanariadha Waislamu wakihakikishwa kupata chakula halali.
Habari ID: 3470499    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/06

Polisi huko Tokyo nchini Japan wanawafanyia ujasusi Waislamu kwa sababu ya dini yao, tokea mwaka 2008.
Habari ID: 3470498    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/06

Wanandoa Waislamu wamelituhumu Shirika la Ndege la Marekani la Delta Airlines kwa kuwa na chuki dhidi ya Uislamu baada ya kuwazuia kusafiri na ndege ya shirika hilo mjini Paris.
Habari ID: 3470497    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/06

Mwanamke Mwislamu aliyekamatwa Uingereza kwa kusoma kitabu kuhusu Syria ameazimia kuwasilisha kesi kulalamikia namna alivyo dhalilishwa na wahudumu wa ndege pamoja na askari wa kupambana na ugaidi.
Habari ID: 3470494    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/04

Jopo la uchunguzi kuhusu mauaji ya Waislamu kaskazini mwa Nigeria limekiri kuwa jeshi la nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika liliuawa Waislamu 348 katika mji wa Zaria jimbo la Kaduna.
Habari ID: 3470492    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/03

Mwanazuoni wa ngazi za juu Iran amempongeza Sheikh Mkuu wa Al Azhar kwa jitihada zake za kuleta umoja wa Waislamu.
Habari ID: 3470490    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/02

Siku kama hii, 25 Mfunguo Mosi Shawwal, miaka 1289 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, Imam Ja'far Swadiq AS mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW aliuawa shahidi kwa kupewa sumu kwa amri ya Mansur Dawaniqi mtawala dhalimu wa Bani Abbas.
Habari ID: 3470485    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/31