Mtuhumiwa alirejeshwa kutoka Italia Ijumaa. Kabla ya kujipeleka kwa mamlaka za Italia kuhusiana na mauaji ya mvulana mwenye umri wa miaka 22 kutoka Mali aitwaye Aboubakar Cissé katika msikiti kusini mwa Ufaransa, mtuhumiwa , aliyetambuliwa kama Olivier A. na vyombo vya habari vya Ufaransa alikuwa mafichoni kwa kwa siku tatu.
Yeye ni raia wa Ufaransa alizaliwa mwaka 2004.
Alisafirishwa kutoka Florence kwenda katika jumba la mahakama katika mji wa Nîmes, kusini mwa Ufaransa, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
Inaripotiwa kuwa anakabiliwa na mashtaka ya "mauaji ya makusudi kutokana na hisia dhidi ya rangi au dini" na "kutoroka baada ya kutenda jinai."
Cissé alishambuliwa na kudungwa kisi mara kadhaa alipokuwa akiswali kwenye msikiti wa mji wa zamani wa uchimbaji wa madini wa La Grand-Combe, kusini mwa Ufaransa.
Olivier A. , na ambaye aliishi katika eneo hilo na ambaye hajaripotiwa kuwa na rekodi ya kihalifu , alichukua video ya mauaji hayo, kisha akaichapisha kwenye Snapchat.
Mauaji ya Cissé yalisababisha mjadala mkali nchini Ufaransa katika wiki zilizopita, ambapo viongozi wa serikali walikosolewa kwa kutotazama tukio hilo kama uhalifu wa chuki na kutoonyesha kiwango cha wasiwasi walichokuwa nacho katika mashambulizi mengine kama hayo nchini humo.
3493009