palestina - Ukurasa 45

IQNA

Rais Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Iran ameashiria pia kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bahrain na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa, watawala wa baadhi ya mataifa ya Kiarabu katika Asia Magharibi hawafungamani na malengo ya taifa madhulumu la Palestina.
Habari ID: 3473176   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/16

TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Al Wifaq ya Bahrain imetangaza ijumaa wiki hii kuwa ni ‘Ijumaa ya Ghadhabu’ kwa ajili ya kubainisha kuchikizwa na mpatano yaliyopfikiwa kati ya utawala haramu wa Israel na utawala wa Bahrain.
Habari ID: 3473175   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/16

TEHRAN (IQNA) – Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas amekosoa vikali utiwaji saini wa mapatano ya uanzishwaji uhusiano wa kawaida baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na utawala haramu wa Israel katika ikulu y White House nchini Marekani.
Habari ID: 3473174   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/16

Shabab Al-Muqawama Global Front Holds Congress
TEHRAN (IQNA) - Kongamano la 7 la Kimataifa la Vijana wa Mapambano (Shabab Al Muqawama) limefanyika Jumatatu nchini Iran kujadili njia za kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473173   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/15

TEHRAN (IQNA) – Qatar imesema katu haitafuata nyao za majirani zake yaani tawala za Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambazo zimeanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473172   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/15

Ayatullah Sheikh Isa Qassim
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Bahrain Ayatullah Sheikh Isa Qassim amesema kuanzisha uhusiano wa kawaida na kati ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kinyume cha matakwa ya wananchi katika nchi hizo.
Habari ID: 3473165   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/13

TEHRAN (IQNA)- Wapalestina wameulaani utawala wa Kifalme wa Bahrain kwa kuanzisha uhusiano na utawala bandia wa Israel.
Habari ID: 3473160   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/12

TEHRAN (IQNA) - Zaidi ya wasomi na wanazuoni 200 wa Kiislamu Jumanne ya jana walitoa fatwa inayoharamisha kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3473154   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/09

TEHRAN (IQNA) - Ismail HaniYa, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameonana ana kwa ana na Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon na kuzungumza naye mambo muhimu yanayohusiana na kambi ya muqawama.
Habari ID: 3473144   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/07

TEHRAN (IQNA) - Wanaharakati wanaounga mkono Palestina wameandamana nje ya uwanja wa mpira wa Hampden Park, huko Glasgow, Scotland nchini Uingereza kulaani mechi iliyochezwa Ijumaa katika ya timu ya taifa ya Scotland na kalbu moja ya soka ya utawala bandia wa Israel.
Habari ID: 3473140   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/05

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniya kwa mara nyingine tena amesisitiza udharura wa kuungana na kushirikiana makundi yote ya kisiasa na kijamii ya Palestina kwa lengo kuzima njama za maadui zao, yaani utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na baadhi ya tawala za kizandiki za Kiarabu.
Habari ID: 3473136   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/04

TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa tena suala la kuanzishwa uhusiano baina ya Imarati na utawala ghasibu wa Israel na kusisitiza kuwa: Jambo lililofanywa na kawaida kwa uhusiano huo ni kubinya shingo la Wapalestina kwa goti la Wazayuni.
Habari ID: 3473132   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/03

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja hatua ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni kuwa ni kuusaliti Ulimwengu wa Kiislamu, Ulimwengu wa Kiarabu na nchi za eneo na kadhia muhimu ya Palestina.
Habari ID: 3473127   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/01

TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok amemfahamisa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo kwamba Khartoum haiwezi kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473103   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/26

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendeleza hujuma zake dhidi ya Ukanda wa Ghaza kwa kuwaua shahidi Wapalestina wanne.
Habari ID: 3473100   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/25

TEHRAN (IQNA) - Wanaharakati wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wameanzisha mkakati wa kupinga uhusiano wa nchi yao na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473095   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/23

Ayatullah Ahmad Jannati
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema kuwa, kuanzisha na kutangaza wazi kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel hakutauwezesha utawala huo ghasibu uendelee kubakia.
Habari ID: 3473086   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/20

TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Tunisia waliokuwa na hasira wameandamana nje ya ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) mjini Tunis kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya UAE na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473085   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/19

TEHRAN (IQNA)- Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas amelaani mapatano ya hivi karibuni yaliyofikiwa ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na utawala haramu wa Israel na kuyataka kuwa ya kipuuzi na yasiyo na maana kwa Wapalestina.
Habari ID: 3473083   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/19

TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kumtia tena mbaroni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina ina lengo la kuwafutilia mbali walinzi wa Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3473077   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/17