iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) amewatumia barua tofauti wakuu na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu zaidi ya 40 akiwataka kuchukua hatua za harakati kusitisha mpango wa Israel wa kutaka kuyaunganisha baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3472852    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/10

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mkono wa pole kufuatia kuaga dunia Katibu Mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihadu Islami ya Palestina, Ramadhan Abdullah Shalah.
Habari ID: 3472847    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/08

TEHRAN (IQNA) -Katibu Mkuu wa zamani Harakati ya Jihad Islami ya Palestina ameaga dunia hospitalini baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Habari ID: 3472844    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/07

TEHRAN (IQAN)- Swala ya Ijumaa imeswaliwa katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) kwa mara ya kwanza jana baada ya msikiti huo kufungwa kwa wiki kadhaa kutokana na janga la COVID-19.
Habari ID: 3472840    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/06

TEHRAN (IQNA) – Maafisa wa kijasusi wa utawala haramu wa Israel Ijumaa walimkamata Imamu wa Msikiti wa Al Aqsa Sheikh Ekrima Sabri akiwa nyumbani kwake Quds (Jerusalem) Mashariki.
Habari ID: 3472814    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/29

TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Palestina katika Ukanda wa Ghaza imesema misikiti ya eneo hilo itafunguliwa tu kwakati wa Swala wa Ijumaa na kwa kuzingatia kanuni za afya za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472811    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/28

Sayyed Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) - Kaitbu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon uwepo wa majeshi ya Marekani katika eneo umetokana na kuimarika nguvu za harakati za mapambano ya Kiislamu au muqawama.
Habari ID: 3472806    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/27

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema hakuna shaka kuwa utawala wa Israel utasambaratika na amesisitiza kuwa, vita asili vitakuwa na Marekani.
Habari ID: 3472793    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/23

Taarifa ya Harakati ya Mshikamano wa Kenya na Palestina
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Mshikamano wa Kenya na Palestina (KPSM) imetoa taarifa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kuwa Wa palestina wanakabiliana na virusi viwili hivi sasa.
Habari ID: 3472792    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/22

Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameielezea Siku ya Kimataifa ya Quds inayoadhimishwa hii leo kote duniani kama utamaduni mzuri na nembo ya uvumilivu, umoja na mshikamano wa Waislamu katika kuhami na kutetea thamani za Kiislamu.
Habari ID: 3472790    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/22

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amelaani vikali jaribio la baadhi za tawala za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3472788    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/21

TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ameutahadharisah vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuchukua hatua zozote dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3472787    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/21

TEHRAN (IQNA) - Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amefuta makubaliano yote yaliyofikiwa kati ya mamlaka hiyo na Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3472786    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/20

Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Intifadha ya taifa la Palestina imeshavuka mipaka ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuingia kwenye awamu itakayoamua hatima yake na akasisitiza kwamba: Minong'ono ya kufikia tamati Israel ghasibu inasikika kwenye mitaa ya Tel Aviv.
Habari ID: 3472784    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/20

TEHRAN (IQNA) - Majlisi ya Ushauri ya Kiisalmu (Bunge la Iran) imeidhinisha muswada wa namna ambavyo Iran itakabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika upeo wa kitaifa na kimataifa.
Habari ID: 3472779    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/19

TEHRAN (IQNA) - Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan ameutahadharisha utawala wa Israel kuwa utaraji mapigano makubwa iwapo utasonga mbele na mpango wake wa kuteka zaidi ardhi za Palestina katika Ukingo wa Magharibi na Bonde la Jordan.
Habari ID: 3472774    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/17

TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje Iran imetoa tamko kuhusu siku ya "Nakba" yaani siku ya nakama ya kuasisiwa utawala pandikizi wa Kizayuni katika ardhi walizoporwa Wa palestina na kusisitiza kuwa, kadhia ya Palestina itaendelea kuwa suala kuu nambari moja katika ulimwengu wa Kiislamu licha ya kufanyika njama nyingi za kulisahaulisha.
Habari ID: 3472767    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/15

TEHRAN (IQNA) – Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu yanatazamiwa kufanyika katika ukumbi wa Instagram na mitandao mingine ya kijamii nchini Afrika Kusini, kutokana na janga la corona.
Habari ID: 3472758    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/12

TEHRAN (IQNA) - Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema Baraza la Usalama la umoja huo limefeli kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel utekeleza maazimio ya baraza hilo kuhusu Palestina na Syria.
Habari ID: 3472699    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/24

Kufuatia janga la corona
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito kwa taasisi za za kisheria Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kuchukua hatua za dharura za kuwaokoa mateka Wa palestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3472675    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/17