iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa wito wa kuanzishwa kamati ya mirengo yote ya Palestina kwa ajili ya kuutetea mji wa Quds Tukufu (Jerusalem) na kuulinda kutokana na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473042    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/07

TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni unatekeleza mashambulizi katika Ukanda wa Ghaza lengo likiwa ni kuwahamishia wananchi wa Palestina migogoro ya ndani ya utawala huo na kupotosha fikra za walimwengu kuhusu matukio na hali mbaya ya kisiasa inayoukabili sasa utawala wa Israel.
Habari ID: 3473028    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/03

TEHRAN (IQNA) -Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ichukue hatua za haraka za kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel hasa kitendo cha utawala huo kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473024    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/02

TEHRAN (IQNA) - Vijana wa Ki palestina wamekabiliana na walowezi wa Kizayuni waliokuwa wakifanya juhudi za kuvamia na kuingia katika Msikiti wa al-Aqswa.
Habari ID: 3473017    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/31

TEHRAN (IQNA) - Mamia ya Wa palestina wameandamana katika Ukanda wa Ghaza kulaani hatua ya mahakama ya utawala haramu wa Israel kufunga lango la Bab al-Rahma la Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3472977    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/19

TEHRAN (IQNA)- Ripota na mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuuzingira Ukanda wa Ghaza kunakofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuwaadhibu kwa umati wananchi wa Palestina.
Habari ID: 3472974    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/18

TEHRAN (IQNA) - Shirika la intaneti la Google limekosolewa vikali watumiaji wa mitandao mbali mbali ya kijamii baada ya kuiondoa "Palestina" katika ramani zake za dunia, na badala yake kupachika jina la "Israel."
Habari ID: 3472970    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/17

TEHRAN (IQNA) - Utawala haramu wa Kizayuni umekusudia kunyakua asilimia 30 zaidi ya ardhi za Palestina za Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan ilizozivamia na kuanza kuzikalia kwa mabavu mwaka 1967 na kuziunganisha na ardhi zingine ilizozipa jina la Israel, ukiwa ni muendelezo wa malengo yake ya muda mrefu ya kuikalia kwa mabavu Palestina yote.
Habari ID: 3472967    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/16

TEHRAN (IQNA) – Wanajeshi wa Utawala wa Kizayuni wa Israel wamwashambulia na kuwafyatulia risasi Wa palestina ambao walikuwa wanashiriki katika mazishi ya M palestina , Ibrahim Mustafa Abu Yakub.
Habari ID: 3472952    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/12

TEHRAN (IQNA) - M palestina ameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472947    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/10

TEHRAN (IQNA) –Mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amepongeza ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas na kusema: “ Ujumbe wa kiongozi wa Iran unaashiria himaya ya kudumu kwa malengo ya Palestina.”
Habari ID: 3472935    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/06

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita hata kidogo katika kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na kuvunja shari za utawala bandia na ghasibu wa Kizayuni.
Habari ID: 3472933    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/06

TEHRAN (IQNA) – Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina za Hamas na Fat'h zimesisitiza kuhusu umoja wa kitaifa za Wa palestina ili kukabiliana na adui mvamizi na ghasibu pamoja, yaani Israel na njama zake ikiwemo ya 'Muamala wa Karne'
Habari ID: 3472925    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/03

TEHRAN (IQNA) - Jumatano Wa palestina walifanya maandamano makubwa dhidi ya utawala haramu wa Israel chini ya anuani ya ‘Siku ya Hasira’ maandamano ambayo yaliungwa mkono kimataifa.
Habari ID: 3472923    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/02

TEHRAN (IQNA) - Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ametoa mwito wa kuchukuliwa hatua athirifu za kukomesha jinai za utawala haramu wa Israel, hususan mpango wa utawala huo ghasibu wa kupora ardhi zaidi za Wa palestina .
Habari ID: 3472922    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/02

TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema nchi yake inapinga hatu aya utawala wa Kizayuni wa Israel kuteka eneo zaidi la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472919    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/01

TEHRAN (IQNA) –Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina (Hamas) amependekeza mfumo mpya wa uongozi wenye kujumuisha wote ili kupatikane umoja wa kitaifa Palestina.
Habari ID: 3472914    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/30

TEHRAN (IQNA) – Harakati za mapambano ya kupigania ukombozi wa Palestina za Hamas na Jihad Islami zimetangaza kuunga mkono harakati za wananchi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya njama za utawala wa Kizayuni za kuteka eneo hilo.
Habari ID: 3472907    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/28

TEHRAN (IQNA)- Israel inashinikizwa na jamii ya kimataifa isitishe mpango wake wa kupora maeneo zaidi ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472895    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/24

TEHRAN (IQNA) –Mamia ya watu wameshiriki katika maandamano mjini Amsterdam Uholanzi Jumapili na kutangaza kuunga mkono Wa palestina huku wakipinga mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel kupora ardhi zaidi za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472865    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/15