TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Ansarullah ya Yemen imesema hatua ya Sudan kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel inalenga kudhamini malengo ya utawala huo ambayo ni kuangamiza taifa la Palestina.
Habari ID: 3473294 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/25
TEHRAN (IQNA)- Makundi ya mapambano ya Kiislamu au muqawama yamelaani vikali hatua ya Sudan kuafiki kuanzisha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel. Wananchi wa Palestina wamekitaja kitendo hicho cha kisaliti kama 'dhambi ya kisiasa.'
Habari ID: 3473290 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/24
Mkuu wa ICRO
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu Iran (ICRO) amesema, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) inapaswa kutekeleza majukumu yake kuhusiana na Fatuwa ambayo imetolewa na wanazuoni wa Kiislamu ya kuharamisha kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473281 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/21
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Ukuras wa Twitter wa Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umezungumzia hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473280 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/21
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Palestina amelaani kitendo cha kuruhusiwa ujumbe wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuingia ndani ya Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) huku Wapalestina wakizuiwa kuswali katika msikiti huo.
Habari ID: 3473279 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/20
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wenye hasira nchini Bahrain wameandamana kupinga safari ya ujumbe wa Marekani-Kizayuni katika nchi yao kwa lengo la kutangaza rasmi mapatano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Bahrain na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473276 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/19
TEHRAN (IQNA) - Asilimia 95 ya wananchi wa Bahrain wanapinga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473272 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/18
TEHRAN (IQNA)- Sayyid Ammar Hakim, Kiongozi wa Mrengo wa Kitaifa wa al-Hikma wa Iraq amelaani vikali siasa za baadhi ya mataifa ya Kiarabu katika eneo la Asia Magharibi za kufanya mapatano na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, nchi yake katu haitafanya mapatano na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3473271 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/18
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel imeupa utawala huo kiburi na ujuba wa kuendelea kupora ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kinyume cha sheria.
Habari ID: 3473268 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/17
TEHRAN (IQNA) – Makumi ya walowezi wa Kizayuni siku ya Alhamisi waliuhujumu uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) wakiwa wanalindwa na askari wa utawala haramu wa Israel ambapo wametekeleza ibada za Kiyahudi katika eneo hilo takatifu la Waislamu.
Habari ID: 3473265 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/16
TEHRAN (IQNA) – Utawala wa Kizayuni wa Israel umeidhinisha ujenzi wa nyumba mpya 2,166 za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3473263 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/15
TEHRAN (IQNA) – Mtaalamu maarufu wa kisiasa Kuwaita amelaani hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na Israel na kutaja hatua hiyo kuwa sawa na ukoloni mamboleo.
Habari ID: 3473257 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/13
TEHRAN (IQNA)- Hali ngumu na isiyo ya kibinadamu ya magereza ya utawala wa Israel imepelekea mateka au wafungwa kadhaa kususia chakula kama njia ya kubainisha malalamiko yao.
Habari ID: 3473252 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/12
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Sudan amekosoa hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema, hatua hiyo ni usaliti kwa kadhia ya Palestina.
Habari ID: 3473243 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/09
TEHRAN (IQNA) – Wasomi wa Kiislamu na wanaharakati katika mirengo kadhaa ya Palestina wamelaani vikali mapatano ya kuanzishwa uhusiano baina ya Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu.
Habari ID: 3473238 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/07
TEHRAN (IQNA) – Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman, ameutembelea utawala wa Kizayuni wa Israel mara kadhaa kwa siri, amefichua afisa wa zamani wa usalama katika utawala huo.
Habari ID: 3473237 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/07
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni umeamua kujenga maelfu ya nyumba za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina unazoendelea kupora huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3473235 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/06
TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Bahrain wameandamana tena Ijumaa katika mji mkuu Manama na miji mingine kupunga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473228 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/03
TEHRAN (IQNA) – Wanaharakati wa kisiasa nchini Tunisia wametaka Oktoba Mosi itambuliwe nchini humo kama ‘Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uzayuni.’
Habari ID: 3473224 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/02
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imepinga madai ya afisa mwandamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa eti utawala bandia wa Israel umesitisha upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni baada ya utawala huo kuanzisha uhusiano na nchi mbili za Kiarabu za UAE na Bahrain.
Habari ID: 3473222 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/02